UMISSETA YAZIDI KUSHIKA KASI TABORA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 17, 2023

UMISSETA YAZIDI KUSHIKA KASI TABORA


Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yameendelea kushika kasi mkoani Tabora, Mikoa ikiendelea kushindandana katika michezo mbalimbali.


Katika mchezo wa Soka Wasichana Mkoa wa Dodoma uliibuka na ushindi mnono baada ya kuifunga Pwani magoli 6-0 katika mchezo uliochezwa uwanja D wa shule ya Sekondari Wasichana Tabora tarehe 17 Juni 2023 saa 4 Asubuhi.


Mchezo mwingine ulipigwa uwanja A wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora, Mkoa wa Mwanza ikikutana na Songwe matokeo yakiwa 2-0, na baadae Kagera wakatoshana nguvu ya 0-0 na Manyara.


Singida na Arusha zilienda Sare ya 2-2, Mtwara ikaifunga Iringa 4-0 na Morogoro ikaenda sare ya 0-0 na Lindi kwenye michezo iliyochezwa saa 2 Asubuhi kwenye viwanja D,C na B.


Kwa upande wa Mchezo wa Mpira wa Wavu Arusha ilishinda Seti 3-1 dhidi ya Pemba, Tanga ikashinda Njombe 3-0, Dodoma ikashinda Songwe 3-0 na Mtwara ikaifunga Mara Seti 3-0 michezo yote ikiwa ilichezwa saa 2 Asubuhi kwenye Viwanja vya shule ya Sekondari Tabora Wavulana.


Katika Mpira wa Netiboli Mkoa wa Mwanza uliadhibu majirani zao shinyanga kwa magoli 45-19, Mbeya ikawafunga Njombe 36-16, Kagera ikafunga Mara 25-29 na wenyeji Tabora wakaishinda Tanga 48-12, michezo yote ikichezwa katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tabora Wasichana.


Michezo mingine Lindi ilikubali kipigo cha 39-11 kutoka kwa Kilimanjaro, Mkoa wa Mtwara ukaifunga Dodoma 37-33 kwenye mchezo uliojaa ufundi, na baadae Arusha ikaifunga Kigoma 34-32.


Mashindano ya UMISSETA 2023 yanayoendelea Mkoani Tabora, yameandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

No comments:

Post a Comment