Na. Gideon Gregory, Dodoma.
NAIBU Waziri wa kilimo na Mbunge wa Dodoma mjini Mh.Antony Mavunde amewataka wanawake wajasiriamali jijini Dodoma kuchangamkia fursa katika biashara pamoja na Kuongeza ujuzi ikiwemo kushiriki semina mbalimbali ili kujifunza na Kuongeza chachu katika kuinua uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo ameitoa Juni 9 Jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya Wanawake wanaweza maarufu kama (SheCanDoIt) yenye lengo la kumuinua mwanamke kiuchumi na kumtoa katika biashara ndogo hadi kumiliki kiwanda kutokana na kuzingatia mafunzo ya semina hiyo.
Amesema serikali imetenga pesa Kwa ajili ya kujenga Jiji la Dodoma hivyo fursa za biashara zitaongezeka kutokana na mji kupanuka na hiyo itawanufaisha wajasiriamali lakini pia serikali imeanzisha Sera itakayo wanufaisha wanawake, watoto na makundi maalumu.
"Serikali kupitia Sheria zake inawapenda sana wanawake na inaitaji mfike mbalii katika kuanzisha biashara na kuja kufikia uchumi wa viwanda na ndio maana Bado fursa zinaongezeka na kuwalenga
ambapo ajira za vijana wazee na watu wenye ulemavu wataweza kunufaika wakiwemo wakina mama kuhusika katika kupata na kuchangamkia frusa za ajira ambapo ni moja ya malengo ya serikali katika Kukuza ajira kwenu"amesema Mh Mavunde.
Akizungumza na OKULY BLOG baada ya mafunzo hayo mlezi wa Vijana na wanawake Tanzania William Machimu amesema kupitia mafunzo hayo wanawake wanatakiwa kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha wanafanya shughuli za kila siku kuwezesha familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kumekuwa na mambo mengi yaliyotokea kama chachu kwa wanawake wote, kwa mfano wamekuwa na kupewa hati kama kielelezo kwamba sasa wameamka na wana uwezo wa kujisimamia hata kama hawatosimamiwa na watu wengine,”amesema.
Pia Machimu ametoa wito kwa wanawake kuwa bado wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko hususani katika uwajibikaji kuchukua hatua za makusudi kutokana na nafasi zilizopo sasa na fursa.
Kwa upande wake Kiongozi na msimamizi wa biashara ya wajasiriamali Bi.Festa Mbunga ametoa elimu Kwa wanawake wajasiriamali ili kukuza biashara zao ambapo amesema katika kuanzisha biashara kunaitajika mipango, maamuzi na maandalizi ya kina ili kuweza kuwa mfanyabiashara endelevu na mkubwa.
"Kwa sasa wajasiriamali wameweza kupata wawekezaji ambao wanawainua wanawake katika kukuza biashara nayo ni Bank na Makundi ya wanawake katika kukuza na kuanzisha biashara hivyo changamkieni frusa, amesema.
Ameongeza "Ni vibaya Kwa mjasiliamali yeyote kuchukuwa mkopo mkubwa ambao upo kinyume na biashara yake na hiyo inakuja badala ya kuingizwa katika ushawishi wa kuchukuwa mkopo usio na malengo.
Naye mjasiriamali wa kujitegemea Bi.zuhura Mkweo amesema semina hiyo imekuwa na faida kwake na kuahidi kuwa ataenda kuwa msimamizi bora wa biashara yake ya kuuza sharubati kutokana na elimu aliyo patiwa.
"Nimejua Jinsi ya Kuongeza mtaji kutoka bank yaani mkopo pia nimepata akili mpya Ya kwenda kutatua changamoto baadhi katika biashara yangu kupitia hapo ntaweza Kuongeza mtaji kuwa mkubwa zaidi.
" Pia ni vyema kuendelea kupenda kazi yetu tunayo ifanya Kwa sababu serikali yetu inatuunga mkono Ili kufikia malengo makubwa kupitia ujasiriamali wa wafanyabiashara wote tukiwemo na sisi wanawake "Zuhura.
No comments:
Post a Comment