WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 29, 2023

WAZIRI SIMBACHAWENE AKUTANA NA WATUMISHI WA SEKRETARIETI YA AJIRA KUHIMIZA UWAJIBIKAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. GeorgeI Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watendaji hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Aliyesimama) akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Meza kuu katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Katikati) na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia) wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa maua ya ukaribisho wakati alipowasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea maua ya ukaribisho mara baada ya kuwasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika taasisi hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuwasili katika ofisi za taasisi hiyo zilizopo jijini Dodoma.

Naibu Katibu, Idara ya Ajira, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Lucas Mrumapili akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete kwa kufanya kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti hiyo ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma mara baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na watumishi hao kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.

No comments:

Post a Comment