BUWSSA YAJIZATITI KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 20, 2023

BUWSSA YAJIZATITI KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI.

Mkurugenzi wa mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Ester Gilyoma, akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) ,leo Julai 20,2023, Jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika Mwaka wa fedha wa 2023/24.
sehemu ya waandishi wa Habari wakimsikiliza, Mkurugenzi wa mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda (BUWSSA) Ester Gilyoma, leo Julai 20,2023, Jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo katika Mwaka wa fedha wa 2023/24.


Na Okuly Julius-Dodoma

Mkurugenzi wa mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda(BUWSSA) Ester Gilyoma ametaja moja ya mkakati wake wa kupunguza upotevu wa maji kuwa ni pamoja na kuweka mita mpya zaidi ya 6000 .


Bi.Gilyoma ameyasema hayo leo 20,2023, Jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya utendaji kazi na muelekeo wa kufikia asilimia 95 ya huduma ya maji Mjini Bunda kwa mwaka 2025 ambapo alisema kuwa upotevu wa maji hasa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni asilimia 36 .


Amesema kuwa wameweka mikakati ya kupunguza upotevu wa maji ulioandaliwa ikiwa ni mpango mkakati wa kupunguza upotevu wa maji wa miaka mitatu ulioanza mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024 unaoendana na mpango wa kibiashara wa Mamlaka ya maji.


Sambamba na hivyo Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda imeandaa andiko mradi kwa ajili ya kukopa fedha kiasi cha TShs 815,000,0000 mfuko wa maji ili kuhakikisha upotevu wa maji unapungua kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024


"Kuna mita ambazo zimekaa miaka 10 mpaka 15 hivyo mita hizi zinatia hasara kwa kiwango kikubwa ,hivyo tumejipanga kwa mwaka huu wa fedha tutaenda kuweka mita 6000 kwani tunapanga kulimaliza jambo hili kabisa " alisema.


Pamoja na hayo alisema kuwa mamlaka hiyo ina uwezo wa kuzalisha maji kutoka kwenye chanzo kipya na cha zamani Nyabehu lita za ujazo 15,264,000 /siku ambayo hayajatibiwa na lita za ujazo 10,320,000/kwa siku ambayo yametibiwa kutoka kwenye chanzo ambacho kimekamilika mwaka 2023.


"Kati ya jumla ya lita za ujazo 10,320,000 Mamlaka ina uwezo wa kuzalisha wastani wa lita 3,870,000 kwa siku kutokana na ufinyu wa mtandao wa bomba kutofika maeneo yote ya Mjini Bunda,hivyo Mamlaka ina akiba ya maji ya kutosha lita za ujazo 6,450,000 yaliyotibiwa na lita za ujazo 4,464,000 kupitia chanzo cha zamani ambazo zinaweza kufikia service coverage ya 95 kufikia Mwaka 2025.


Mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa sasa Mamlaka hiyo haina huduma ya majitaka,hivyo magari ya watu binafsi ambayo yanasimamiwa na Halmashauri ya mji wa Bunda ndiyo yanatumika katika kutoa huduma za majitaka.


" Hivyo kupitia Mamlaka ya maji Bunda kwa mwaka wa fedha 2023/2024 tunategemea kuanza kujenga miundo mbinu ya majitaka eneo la Butakale liliyoko Mjini Bunda"alisema


Pia amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Bunda ina jumla ya wateja 7,556 kati ya hao kuna wateja wa Nyumbani,Taasisi na Biashara.


Aidha mlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Bunda inatumia maji toka chanzo cha ziwa Victoria, chanzo hicho ni cha uhakika kiko eneo la Nyabehu umbali wa Km 24.8 toka Bunda Mjini.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo amewataka wananchi wa Bunda kuendelea kuilinda miundombinu hiyo ya maji kwani imegharamiwa kwa fedha nyingi hivyo inastahili kutunzwa vyema ili iwatunze.


"Natoa rai kwa wanaoiba maji kuacha mara moja kwani jambo hilo limepitwa na wakati ,lakini pia linachangia kupoteza kwa mapato ya ndani jambo ambalo halikubaliki" alisema.

No comments:

Post a Comment