Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga (katikati ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi)
Vikundi vya mazoezi ya viungo Mkoa wa Shinyanga na Mwanza (Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC), Kahama Jogging Club na Isamilo Jogging) vimefanya bonanza la michezo Mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka minane tangu kuanzishwa kwa PJFC.
Bonanza hilo likiongozwa na kauli mbiu “Kataa uhalifu toa taarifa, Shinyanga bila uhalifu inawezekana” limefanyika leo Jumamosi Julai 15,2023 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo mbio za mita 100 na 200, mpira wa miguu, kufukuza kuku, mbio za magunia na kuvuta kamba.
Awali kabla ya michezo hiyo, wafanya mazoezi hao Kahama Jogging Club, PJFC na Isamilo Jogging Club pamoja na Askari Polisi Mkoa wa Shinyanga na Vijana wa hamasa CCM walifanya mazoezi ya kukimbia (Jogging) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kuanzia Bwalo la Polisi Mjini Shinyanga kupitia mitaa mbalimbali kisha kumalizia mbio hizo katika viwanja vya Shy Com.
Akizungumza wakati wa Bonanza hilo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amevipongeza vikundi hivyo vya mazoezi kwa ushirikiano huku akisisitiza jamii kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kuepuka tabia bwete ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
“Hongereni PJFC kwa kuwakaribisha Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club kuja hapa Shinyanga, hii yote ni katika kujenga mahusiano lakini pia kuimarisha afya ya mwili na akili”,amesema Mhe. Samizi.
“Michezo inajenga afya ya mwili na akili, na ukiona umechanganyikiwa fanya mazoezi. Tufanye mazoezi, tuache tabia bwete ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza”,ameongeza.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wafanya mazoezi hao pamoja na jamii kwa ujumla kupinga na kuzuia ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Emmanuel Christian Galiyamoshi ameishukuru jamii kwa ushirikiano inaotoa kwa jeshi la polisi katika kuzuia matukio ya uhalifu.
“Tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano mnaotoa kwa jeshi la polisi katika kukataa uhalifu kwa kutoa taarifa. Wafanya mazoezi nyinyi ni kama askari polisi, polisi ni wachache hivyo endeleeni kushirikiana nasi ili kupunguza uhalifu katika jamii na tutahakikisha tunaongeza wafanya mazoezi hadi ngazi za vijiji”,amesema Galiyamoshi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na kikundi cha mazoezi ya viungo maarufu Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) ambalo limeshirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club leo Jumamosi Julai 15,2023 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na kikundi cha mazoezi ya viungo maarufu Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) ambalo limeshirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Emmanuel Christian Galiyamoshi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na kikundi cha mazoezi ya viungo maarufu Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) ambalo limeshirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club

Vikundi vya mazoezi ya viungo maarufu Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC), Kahama Jogging Club na Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza wakiwa nje ya Bwalo la Polisi Mjini Shinyanga wakijiandaa kuanza kukimbia (Jogging) Mitaa mbalimbali Mjini Shinyanga.
Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga (katikati ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi)
Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC), vijana wa hamasa CCM wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Vijana wa hamasa CCM wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Vikundi vya mazoezi ya viungo - Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC), Kahama Jogging Club na Isamilo Jogging Club wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Vikundi vya mazoezi ya viungo - Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC), Kahama Jogging Club na Isamilo Jogging Club wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga. Mbele ni Isamilo Jogging Club wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Askari polisi Shinyanga wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Askari polisi Shinyanga wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Kahama Jogging Club wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Mazoezi yanaendelea
Mazoezi yanaendelea
Mazoezi yanaendelea
Mazoezi yanaendelea
Vijana wa hamasa CCM wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Askari polisi Shinyanga wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Isamilo Jogging Club wakifanya mazoezi Mjini Shinyanga
Mazoezi yakiendelea katika viwanja vya Shy Com
Mbio za mita 100 zikiendelea wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na PJFC likishirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club

Mbio za magunia zikiendelea wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na PJFC likishirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club
Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea wakati wa Bonanza la Michezo lililoandaliwa na PJFC likishirikisha pia Isamilo Jogging Club kutoka Jijini Mwanza na Kahama Jogging Club

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati), viongozi na askari polisi wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati), viongozi na Isamilo Jogging Club wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati), viongozi na Kahama Jogging Club wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati), viongozi na Shinyanga Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) wakipiga picha ya kumbukumbu
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (katikati), viongozi na vijana wa hamasa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments:
Post a Comment