Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu Julai 14,2023,anatarajiwa kufungua mashindano ya kimichezo yatakayozikutanisha shule zote za Sekondari zilizopo katika jimbo hilo.
Katika hafla hiyo Mbunge Mtaturu anatarajia kugawa vifaa vya Michezo (Mipira na Sare) kwa timu zote 19 zitakazoshiriki mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Julai 14,mwaka huu katika uwanja wa shule ya Sekondari Ikungi.
Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza majira saa 8:00 Mchana yanatarajiwa kuzikutanisha timu za mpira wa Miguu na Mpira wa pete na yatabeba ujumbe usemao*"Michezo & Elimu ni Mapacha"* ili kuhimiza ushiriki wa Michezo na kukuza stadi za Kielimu.
No comments:
Post a Comment