Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam
WAFANYABIASHARA wadogo, wakati na wajasiriamali wameshauriwa kutembelea banda la Mfuko wa Self lililopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam(DITF),maarufu Saba Saba, yenye kaulimbiu isemayo"Tanzania Mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji,".
Akizungumza jijini Julai 03, 2023, Dar es salaam katika maonesho hayo Meneja Masoko na Uhamashishaji Mfuko wa Self, Linda Mshana amesema
mfuko huo una mikopo kwa ajili ya wafanyakazi wa taasisi za serikali ambao wanataka kuboresha makazi yao, wakulima na Wazabuni katika Kampuni binafisi za aina mbalimbali hapa nchini.
Ameongeza kuwa ni wakati muhimu wa kuongeza Uwekezaji katika nchi hivyo wajasiriamali wenye vikundi, na wale wenye namba ya utambulisho ya mlipa Kodi (TIN NUMBER),wanakaribishwa.
"Tupo hapa ndani ya banda la Wizara ya Fedha na mipango tukitoa huduma mbalimbali kwa ajili ya wananchi tunawakaribisha kuja kutembelea banda letu mnaweza kupata fursa ambazo tunazitoa katika mfuko huu, tuna mikopo ya aina mbalimbali kwa wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa," amesema.
Aidha amewataka wananchi watakapopata nafasi ya kufika katika banda hilo wachukue fursa ya kuuliza maswali yote waliyonayo na kwamba riba zao ni nafuu hakuna mtanzania atakaye shindwa kupata mkopo huo kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.
No comments:
Post a Comment