Na Okuly Julius-Dodoma
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe amewataka Walimu Wakuu na Waratibu wa ndani ya Shule kuwasaidia na kuwawezesha wanafunzi kushiriki katika Mashindano ya Uandishi wa Insha.
Pia amewataka kuwasaidia wanafunzi kufuata miongozo iliyowekwa ya Uandishi wa Insha ili Insha nzuri za wanafunzi zipatikane katika Mashindano, Kwa kuwa kushindwa kufuata miongozo ya Uandishi wa Insha kunasababisha Insha hizo ziondolewe wakati wa usahihishaji ngazi ya Taifa.
Prof.mdoe ameyasema hayo Leo Julai 15,2023, Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kutunuku zawadi Kwa washindi wa Kitaifa wa shindano la Uandishi wa insha za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusaini Mwa Afrika (SADC) Mwaka 2021.
Amesema umuhimu wa kushiriki Mashindano hayo Kwa wanafunzi ni kuwaongezea uwezo katika kukuza ujuzi wa lugha,unawaongezea maarifa Kwa ujumla Kwa kupata uelewa wa mada mbalimbali za masomo mengine na kuwasaidia Kwa siku za usoni kunufaika na mtangamano wa Jumuiya hizi.
"Umuhimu wa kushiriki Mashindano kama haya na mengine hutoa Fursa Kwa wanafunzi kutumia Muda wao Kwa masuala muhimu na hivyo kujiepusha na Vitendo visivyofaa na pia Kwa wanafunzi wanaoshinda hujiongezea kipato na kuwezesha Shule zilizotoa washindi watatu wa kwanza katika shindano la Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata vifaa mbalimbali,"
Na kuongeza kuwa"Uandishi wa Insha unawapa wanafunzi Fursa ya kutafiti na kupata taarifa zaidi, kuelewa na kuwawezesha kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na Jumuiya zetu na husaidia wanafunzi wa Kitanzania kuchanganua masuala kutoka nyanja mbalimbali na kulinganisha nyanja hizo na Mazingira yetu,"Amesema Prof Mdoe
Kwa upande wake Alfred Kazimoto ambaye amezungumza Kwa niaba ya Katibu Mkuu OR-TAMISEMI amesema kuwa Mashindano hayo yatawasaidia wanafunzi walioshiriki kujibu vyema mitihani yao ya mwisho kwani tayari wamepata uzoefu Mkubwa.
"Mashindano haya ni muhimu sana Kwa wanafunzi wetu kwani kutokana na utafiti walioufanya ili kupata Cha kuandika katika Insha zao hivyo tunaamini wamesoma vitu vingi ambavyo mwisho wa siku zitawasaidia katika kujibu baadhi ya mitihani yao,"Amesema Kazimoto
Amesema kuwa Jumla ya wanafunzi 133 walishiriki katika shindano la uandishi wa Insha za SADC Kwa Mwaka 2021 na baada ya usahihishaji wakapatikana washindi 10 katika ngazi ya Taifa ambao wamepewa zawadi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo zawadi zilikuwa zikitolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu tu.
" Kwa upande wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki washiriki walikuwa 315 Kwa Mwaka wa 2021 ambapo baada ya usahihishaji wakapatikana washindi 10 ambao wamegawanywa katika Makundi mawili A na B,
Na kuongeza kuwa "Kundi A wanapewa zawadi tofauti tofauti kulingana na nafasi ya ushindi kitaifa na kundi B ni mshindi kuanzia nafasi ya Sita hadi kumi Hawa wanapewa zawadi zinazofanana kutoka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,"amefafanua Masati
Katika mchakato huo wa kupatikana Kwa washindi wa shindano hilo ,Insha za wanafunzi ziliwasilishwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia baada ya kuteuliwa Insha bora katika ngazi ya Shule na kusahihishwa na jopo la wataalamu, ambapo Kwa zile za Jumuiya ya Afrika Mashariki Zoezi Hilo lilisimamamiwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Zile za SADC husimamiwa na Wizara ya Elimu Tanzania Bara na Zanzibar.
No comments:
Post a Comment