Na Okuly Julius-Dodoma
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania(TFRA) Dkt. Stephan Ngailo wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/24 ambapo amesema malengo ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji mbolea kwa nchi za afrika mashariki.
Katika hatua nyingine Dkt. Stephan Ngailo amesema vipaombele vya mamlaka hiyo ya (TFRA) ni kuendelea kudhibiti ubora wa mbolea, kuhamasisha uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vya kuzalisha mbolea na kuimarisha utoaji huduma bora kwa wakulima.
Pia amesema ili kufanikisha Ajenda 10/30 na Kilimo ni biashara Dkt Ngailo amebainisha kuwa Mamlaka hiyo itahakikisha ajenda na maono hayo yanafikiwa kwa kuimarisha upatikanaji na usambazaji wa mbolea bora kwa wakati na kwa bei himilivu.
Kwa ujumla, lengo la sera ni kuendeleza sekta ya kilimo yenye ufanisi, ushindani na faida Hivyo kuboresha maisha ya Watanzania na kufikia ukuaji mpana wa uchumi na kupunguza
umaskini
"Hivyo, kuongezeka kwa matumizi ya pembejeo za kisasa
(mbolea, kemikali za kilimo, mbegu, mashine za kilimo)
ni muhimukwa uzalishaji wenye tija, kuimarisha usalama
wa chakula na kupunguza umaskini" ameeleza Dkt.Ngailo
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya
Kilimo iliyoanzishwa na sheria ya Mbolea Namba 9 ya Mwaka 2009 (Fertilizer Act, 2009) na kanuni zake
za Mwaka 2011 na ilianza kutekeleza majukumu yake
mnamo Agosti 2012.
No comments:
Post a Comment