UTAFITI UTASAIDIA KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO-DKT.JINGU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 19, 2023

UTAFITI UTASAIDIA KUPAMBANA NA UKATILI DHIDI YA WATOTO-DKT.JINGU

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu,akizungumza Leo Julai 19,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024.
Mkurugenzi Msaidizi huduma za ustawi wa jamii kutoka OR-TAMISEMI, Bi.Subisya Kabuje,akizungumza Leo Julai 19,2023 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024.
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024, Jijini Dodoma Leo Julai 19,2023
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024, Jijini Dodoma Leo Julai 19,2023
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024, Jijini Dodoma Leo Julai 19,2023
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024, Jijini Dodoma Leo Julai 19,2023
Mkurugenzi wa Shirika la THPS Dkt.Redempta Mbatia,akizungumza Leo Julai 19,2023 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024.

Na Okuly Julius-Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.John Jingu amesema njia nzuri ya Kupambana na ukatili dhidi ya watoto ni kufanya utafiti ili kujua ukubwa wa tatizo Hilo na njia sahihi ya Kupambana nalo.


Dkt.Jingu ameyasema hayo Leo Julai 19,2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa masuala ya Watoto wenye lengo la kujadili utafiti wa ukatili dhidi ya Watoto (VACS) 2024.


"Ili kuweza kufanya jambo lolote Kwa usahihi ni lazima ulijue hilo jambo Kwa undani hivyo ili tuweze Kupambana na ukatili wa Watoto ni lazima tufanye utafiti wake tujue ukubwa wa tatizo ndipo tupambane nalo na ikiwezekana kutokomeza kabisa,


Na kuongeza kuwa"Rasilimali muhimu kuliko zote katika taifa hili ni Watoto hivyo ni lazima tuwalinde Kwa namna yeyote Ile Kwa kuhakikisha afua zote za kumlinda mtoto dhidi ya ukatili zinafanyiwa kazi bila kufumbia Macho,"amesema Dkt.Jingu


Dkt.Jingu amesema kutokana na Takwimu za WHO ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa watoto bilioni 1 wamefanyiwa ukatili huku asilimia hamsini ya ukatili huo umefanyika katika Bara la Afrika na kusisitiza kuwa jambo Hilo halikubaliki ndio maana Wadau wanaendelea kuungana Kwa pamoja kufanya tafiti itakayotoa majibu ni wapi tunaelekea na kazi inayotakiwa kufanyika ili kukomesha Vitendo hivyo.


Kwa upande wa Mkurugenzi Msaidizi huduma za ustawi wa jamii kutoka OR-TAMISEMI, Bi.Subisya Kabuje, amewataka Wadau wanotekeleza utafiti huo kuhakikisha wanaweka usiri wa mahojiano yao na watoto na kuwatumia Wataalamu wakati wakitekeleza Zoezi hilo ili kuwasaidia watoto waliofanyiwa ukatili kuwa sawa Kisaikolojia.


"Tujitahidi kuhifadhi Siri za Mtoto wakati tunakwenda kuwafanyia mahojiano watoto,tuwashirikishe wataalamu ili Kwa wale watoto waliofanyiwa Ukatili watengenezwe kisaikolojia,"amesema Kabuje


Naye Meneja wa Methodolojia za Takwimu na uratibu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Emilian Karugendo amesema moja ya nguzo katika kukusanya taarifa ya Mtu mmoja mmoja ni usiri hivyo hazitakiwi kutoka Kwa namna yeyote Ile.

Pia ametoa wito Kwa wadau kuhakikisha wanatumia Takwimu hizo Kwa malengo yaliyokusudia Huku akiahidi kuwa ofisi ya Takwimu Tanzania na Visiwani ipo tayari kutoa ushirikiano wowote Kwa wadau kadiri watakavyouhitaji.


Mkurugenzi wa Shirika la THPS Dkt.Redempta Mbatia amesema katika Mkutano huo watapata nafasi ya kujadiliana ukubwa wa utafiti,umuhimu wa utafiti na majukumu ya Kila Mdau katika kutekeleza utafiti wenyewe hivyo baada ya utafiti huo watajua ukubwa wa tatizo Kwa wanaamini matukio yanayoripotiwa ni machache kuliko Yale ambayo hayaripotiwi.


"Utafiti tutakaoufanya utatusaidia kujua MATUKIO mengi zaidi ya ukatili wa Watoto ambayo huenda mengi ya hayo hayajaripotiwa,"Dkt.Mbatia

No comments:

Post a Comment