DAWASA KUTUMIA BILIONI 425.9 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 11, 2023

DAWASA KUTUMIA BILIONI 425.9 KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI


Na Okuly Julius-Dodoma

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), imesema katika kipindi cha mwaka 2023/20 24,imepanga kutekeleza miradi ya kimkakati saba itakayogharimu Shilingi Bilioni 425.9.


Miradi hiyo ni pamoja na bwawa la Kidunda, ujenzi wa mtambo wa kuzalisha maji wa Rufiji,Kwala, Pangani Kibaha, Kimbiji-Kigamboni hadi jirani na Chuo cha Uhasibu (TIA), Kusini
mwa Jiji la Dar es salaam na uchimbaji visima virefu tisa eneo la Kigamboni.


Hayo yameelezwa Leo Agosti 11,2023 Jijini Dodoma na Kaimu Ofisa Mtendaji mkuu wa Mamlaka hiyo, Kiula Kingu wakati akielezea shughuli mbalimbali za DAWASA na mwelekeo wa utekelezaji wa Miradi KATIKA Mwaka wa fedha wa 2023/2024


Ambapo Kaimu Mkurugenzi huyo,amesema kuwa miradi hiyo inalenga kuongeza wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA, kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji.


"Miradi hii itakayotekelezwa kwa jumla ya Tsh. Bilioni 425.9 ina inalenga katika; kuongeza
wingi wa maji yanayozalishwa na DAWASA, kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji,
kuimarisha mfumo wa usambazaji maji na kuimarisha huduma katika maeneo ambayo
hayana mtandao hasa yale ya pembezoni,"amesema Kingu


Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maji katika mwaka 2022/2023,Kingu amesema wamewekeza miradi mikubwa 96 ikiwemo 10 ya kimkakati yenye thamani ya Shilingi Bilioni 219.


Kingu amesema kwa upande wa majitaka wamemewafikia wateja kwa asilimia 43 na hivyo kupunguza changamoto ya ugonjwa wa kipindupindu.

DAWASA ina jumla ya mikoa kazi 23 yenye jumla ya wateja 420,000 ambapo kiasi cha maji kinachozalishwa kwa siku ni lita milioni 590 ambapo kiasi cha mahitaji ya maji kwa siku ni lita milioni 544.





No comments:

Post a Comment