Na Okuly Julius-Dodoma
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha Tano Mwaka 2023 ni 130446 ambapo kati yao 125402 ni Shule za Bweni na 5044 ni Shule za kutwa na Shule za sekondary za kidato Cha Tano ni 548 ambapo kati ya Shule hizo 31 ni za Kutwa.
Msonde ametoa kauli hiyo Leo Agosti 12,2023 Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma wakati wa Ziara yake ya kukagua maandalizi ya Shule za Mkoa huo za kupokea wanafunzi wa kidato Cha Tano.
"Niwatake wazazi na walezi kuhakikisha watoto wetu waliopangiwa kidato Cha Tano wanaripoti katika Shule walizopangiwa Kwa wakati ili waanze masomo Kwa wakati tena Kwa pamoja ili wasipishane katika Masomo,"
Na kuongeza" kuhusu wanafunzi walioomba kuhamia shule nyingine nikiri tu kuwa maombi yao yamepokelewa ila Kwa sasa ni lazima waripoti katika Shule walizopangiwa angalau ndani ya Mitatu hivi kama nafasi zitatokea wataruhusiwa kuhamia kule walipoomba kama nafasi zitapatikana,"amesema Msonde
Pia Dkt.Msonde amewataka Wakuu wa Shule kuwabadilishia tahasusi wanafunzi walioomba ila wazingatie vigezo vilivyowekwa na OR-TAMISEMI na kama hakuna tahasusi hiyo katika Shule husika mwanafunzi anapaswa kuandika barua kwenda Kwa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ili kupelekwa katika Shule husika kama nafasi ikitokea ndani ya miezi miwili.
"Ni sawa Mwanafunzi kuomba kusoma tahasusi anayoipenda ndio maana tuliwapa Uhuru wa kuomba kubadilishiwa ila ni lazima awe na vigezo vilivyopendekezwa ila natamani kuona wengi wakiomba kubadili tahasusi kwenda kusoma masomo ya Sayansi.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Gifti Kyando ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita Kwa uamuzi wa kutoa fedha Kwa ajili ya kuboresha na kujenga miundombinu Mpya Katika Shule za Sekondari hasa zile ambazo zinawapokea wanafunzi wa kidato Cha Tano 2023
"Sisi kama Mkoa wa Dodoma tupo tayari kuwapokea wanafunzi wote tuliopangiwa katika Shule zetu Kwa sababu kama ni madarasa,mabweni na Matundu ya vyoo vyote vipo tayari kabisa Kwa ajili ya kuwapokea na walimu wamejipanga vizuri Kwa ajili ya kuwafundisha na kuwalea Hawa watoto kwani tunajua wengi wanatoka nje ya Dodoma hivyo ni wageni wa Mazingira,"amesema Kyando
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Dkt.Omary Nkullo ameahidi kuwa fedha zote zilizopelekwa katika Wilaya hiyo Kwa ajili ya kutekeleza Ujenzi wa Miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu ya Shule.
Mkoa wa Dodoma Kwa Mwaka 2023 wamepangiwa kupokea wanafunzi wanaojiunga na kidato Cha Tano 5863 ambao wamegawanywa katika Shule 22
No comments:
Post a Comment