HAKUNA KIWANDA KITAKACHOFUNGWA-DKT.KIJAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, August 3, 2023

HAKUNA KIWANDA KITAKACHOFUNGWA-DKT.KIJAJI


Waziri wa Viwanda Na Bishara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali inahakikisha sekta binafsi inaendelea kukua na hakuna kiwanda chochote kitakachofungwa ili kuendelea kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Taifa


Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha A to Z kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji kiwandani hapo na kusikiliza na kitatua changamoto walizonazo.


Aidha, Amewataka wafanyabiashara kuwa na ushirikiano na Serikali katika kutoa changamoto wanazozipata na watoe mapendekezo ya suluhisho za changamoto hizo kwa kuwa Serikali ipo tayari kuzishughulikia


No comments:

Post a Comment