Na Mwandishi wetu - Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka ameitaka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kutoa mafunzo kwa wafanyakazi sekta ya umma na binafsi ili kuepusha kesi zinazojirudia mahali pa kazi.
Aidha, Mhe. Mtaka amesema kuwa migogoro na mivutano ambayo inajitokeza katika maeneo ya kazi inakwamisha utekelezaji wa majukumu, hivyo ameshauri tume hiyo kutoa mafunzo kuhusu utatuzi wa migogoro na taratibu za kufanya uamuzi wa kesi wanazopokea ili mahali pa kazi kuwe na tija.
Ameeleza hayo Agosti 4, 2023 alipotembelea banda la Tume ya Usuluhishi na Uamuzi katika maonesho ya siku ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.
“Fanyeni mapitio ya kesi zinazoletwa kwenu na muangalie makosa yanayo jirudia rudia ili mshirikiane na watumishi wa Utumishi kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kazi katika sekta zote ili kuepusha kesi zinazojirudia rudia “ amesema Mtaka
No comments:
Post a Comment