SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI-DKT.KIJAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 2, 2023

SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI-DKT.KIJAJI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali inatekeleza jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kutatua changamoto walizonazo.


Dkt. Kijaji amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Magodoro cha TANFOAM kilichopo Jijini Arusha kujionea shughuli za uzalishaji magodoro na kisikiliza changamoto walizonazo.


Aidha, Amesema Wizara yake inatekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambapo moja msingi yake ni kuondoa majukumu yanayofanana kati ya Taasisi ili kurahisisha ufanyaji biashara na uwekezaji nchini


Akiongea na uongozi wa kiwanda hicho, Dkt. Kijaji amezitaka Taasisi kuacha kufanya majukumu yanayofanana na kuzitaka kushirikiana katika kuwahudumia wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza biashara na uchumi wa Taifa


Naye Mkurugenzi Msaidizi wa TANFOAM Bw Mechack Jimmy ameishukuru Serikali kwa jitahada mbalimbali inazozifanya katika kutatua changamoto za Wafanyabiashara na wawekezaji ili kuwawekea mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment