SERIKALI HAIPO TAYARI KUWAKWAMISHA WAFANYABIASHARA- DKT.KIJAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 2, 2023

SERIKALI HAIPO TAYARI KUWAKWAMISHA WAFANYABIASHARA- DKT.KIJAJI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao bali itawasaidia kukua na kuendelea kibiashara, kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha ufanyaji biashara wao unakuwa na tija na manufaa kwa Taifa .


Amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vishikwambi cha Tanztech kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza changamoto zao.


Aidha Dkt. Kijaji amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA katika mitaala ya elimu


Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho cha Tanztech Bw. Gurveer Hans amesema Kiwanda hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutoa bidhaa hiyo mashuleni na kwa watu binafsi kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment