DKT.KIJAJI AKITAKA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI KILIMANJARO KUONGEZA UZALISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, August 2, 2023

DKT.KIJAJI AKITAKA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI KILIMANJARO KUONGEZA UZALISHAJI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili ziweze kukudhi mahitaji ya soko la ndani na soko la nje.


Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kitatua changamoto zilipo kiwandani hapo.


Aidha, Dkt Kijaji amesema bidhaa hizo kama Viatu, mabegi na mapochi zinazotengenezwa na Kiwanda hicho kwa kitumia malighafi za ndani ya nchi zina asilimia 100 ya kukishi vigezo vya kuingia katika soko la eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA).

No comments:

Post a Comment