Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi mitungi ya gesi kwa Watu Wenye Ulemavu katika Wilaya ya Hai wakati wa ziara yake katika Mkoa huo. |
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Ummy Nderiananga akikabidhi fimbo nyeupe kwa wasiyoona katika Wilaya ya Hai wakati wa ziara yake Mkoani humo. |
Baadhi ya watu wenye ulemavu katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo. |
Baadhi ya watu wenye ulemavu katika Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo. |
Na Mwandishi wetu- Kilimanjaro
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Ummy Nderiananga ameunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha watu wenye ulemavu na vikundi vya wanawake kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutoa Mitungi ya gesi.
Mhe. Ummy ametoa mitungi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro huku akisisitiza umuhimu wa nishati hiyo mbadala ambapo amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imelenga kuhakikisha inapunguza matumizi ya kuni, mkaa ili kulinda afya za wananchi.
Amesema kuwa licha ya athari za kimazingira zinazotokana na ukataji wa miti unaofanywa na Wananchi Matumizi ya nishati chafu yamekuwa na athari zaidi za kiafya.
“Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi katika maeneo mengi ikiwemo programu ya kumtua mama ndoo kichwani lakini akasema wakina mama wanapata shida wao ndio wapishi sasa ni wakati wa kuwatua kuni kichwani kwa kuwasaidia kupata nishati ya gesi na mimi nimekuja kutekeleza adhma yake ya kumtua mama kuni kichwani” Amesema Mhe.Ummy
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Watu Wenye Ulemavu nchini kutumia fursa ya uanzishwaji wa Vyuo Vya Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu ili kupata elimu ya ujuzi itakayowawezesha kujikwamua kimaisha na kuondokana na hali ya utegemezi.
“Ni muhimu kwa wazazi na walezi wenye vijana wenye ulemavu kuwapeleka na kuwaandikisha katika vyuo vilivyopo Kikanda kupata elimu itakayowajenga kujitegemea kutokana na fani mbalimbali zinazotolewa ikiwemo Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu (Kanda ya Kaskazini kilichopo mtaa wa Masiwani Mkoani Tanga,”Ameeleza.
Awali Akiwasilisha taarifa kuhusu watu wenye ulemavu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bwa. Robert Mwanga alibainisha kwamba Wilaya ya Hai imefanikiwa kuwawezesha watu wenye ulemavu, wanawake na vijana kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri ambayo ilikuwa inatolewa katika kila Halmashauri Nchi nzima.
“Wanawake, vijana na wenye ulemavu wameboresha mitaji yao na kuanzisha shughuli za uzalishaji mali na biashara, kupata huduma za kijami kama maji, elimu na afya. Pia tumeendelea kutoa elimu ya fedha, utunzaji wa kumbukumbu kupitia semina ambazo hutolewa na Halmashauri pamoja na kutoa ajira kwa wenye ulemavu 827,”Alieleza Bwa. Mwanga.
Naye Mbunge wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro Mhe. Saasisha Mafue alipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendela kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu na maji.
“Ipo miradi mingi sana inatekelezwa na Serikali na kwa elimu ni ujenzi wa shule kama Machame Girls imepokea Milioni 300, Harambee Milioni 487, Ryamungo Milioni 200 miradi ambayo mkandarasi yupo site yote haya yanafanyika kutokana na nia njema ya Rais wetu,”Alifafanua Mbunge huyo.
No comments:
Post a Comment