TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUUWA NCHI WANACHAMA KUTOKA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 5, 2023

TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO MKUU WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUUWA NCHI WANACHAMA KUTOKA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma (kushoto) ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wawakilishi wakifuatilia kikao kuhusu maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.
Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wawakilishi wakifuatilia kikao kuhusu maandalizi ya  Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika kilichofanyika leo tarehe 05, Septemba 2023 Jijini Dodoma.

Na Mwandishi wetu- Dodoma  

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023.


Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa.


Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi wanachama wa jukwaa hilo ni pamoja na Kenya, Uganda, Namibia, Zimbabwe, Eswatini, Msumbiji, Seychelles, Botswana.


Nchi nyingine ni Angola, Zanzibar, Malawi, Lesotho, Mauritius, Zambia na Afrika ya Kusini ambapo mkutano huo utafanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Jukumu la Mahakama za Nchi Wanachama katika Utatuzi wa Migogoro chini ya Utangamano wa eneo Huru la Biashara la Afrika: Matumizi ya Teknolojia ya Kisasa kwa Ufanisi katika Utoaji Haki”

No comments:

Post a Comment