TAASISI YA ISLAMIC HELP TANZANIA KUJENGA CHUO CHA AFYA HANDENI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 18, 2023

TAASISI YA ISLAMIC HELP TANZANIA KUJENGA CHUO CHA AFYA HANDENI.


Na.WAF

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu Bw. Zubery Tittee kutoka Taasisi ya Islamic Help Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Afya katika Wilaya ya Handeni, Tanga.

Waziri Ummy Mwalimu ameipongeza Taasisi hiyo kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali kwa vitendo na kusogeza maendeleo karibu na wananchi katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu na Maji pamoja na miundombinu ya kutolea huduma za kijamii


“Nawapongeza Islamic Help Tanzania kwa kuamua kujenga Chuo cha Afya katika Wilaya ya Handeni, chou hiki kitasaidia katika kuzalisha wataalam wa afya na sisi Wizara ya Afya tunaahidi kushirikiana nanyi kufanikisha jambo hili ili kuleta tija kwa watanzania ” ameeleza Waziri Ummy

Bw. Zubery amesema kuwa Taasisi ya Islamic Help Tanzania imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za kijamii na tayari wameshashirikiana na Serikali katika Ujenzi wa Hospitali ya Handeni iliiyogharimu zaidi ya Bilioni 3 pamoja uboreshaji wa miundombinu ya Vituo vya Afya nchini.

No comments:

Post a Comment