WAZIRI NAPE AFUNGUA KONGAMANO LA 7 LA TEHAMA NCHINI - TAIC2023 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 18, 2023

WAZIRI NAPE AFUNGUA KONGAMANO LA 7 LA TEHAMA NCHINI - TAIC2023


Leo Oktoba 18,2023, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amefungua rasmi Kongamano la 7 la TEHAMA Nchini (TAIC2023) lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa TEHAMA ilianza tarehe 16 Oktoba, 2023 na kutarajiwa kuhitimishwa tarehe 20 Oktoba, 2023.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni: Kuibua teknolojia zinazoibukia za kidijitali katika mageuzi ya kidijitali kwa ajili ya kubuni nafasi za kazi na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Mobhare Matinyi (wa kwanza kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa (wa katikati) mara baada ya kufungua Kongamano la 7 la TEHAMA Nchini (TAIC2023) lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, leo Oktoba 18, 2023.

Bw. Gerson Msigwa ndiye aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali kabla ya kuteuliwa na Rais kuwa Katibu Mkuu.

No comments:

Post a Comment