Waziri wa Ujenzi Mh.Innocent Bashungwa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Mohammed Besta kukamilisha usanifu wa kina wa Barabara ya Mkata- Kwamsisi KM 36, ifikakapo desemba 31 mwaka huu.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua athari za mvua za vuli Mkoani Tanga leo Mh. Bashungwa amesema fedha za mradi huo zipo tayari hivyo kinchotakiwa kazi ya usanifu ifanyike haraka ili ujenzi uanze maramoja.
"Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameashatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara hii hivyo kazi ya usanifu ikikamilika ujenzi uaanze haraka," amesisitiza Bashungwa.
Amezungumzia umuhimu wa Watendaji wa TANROADS wa ngazi zote kushirikiana na Mamlaka za Serikali ya mitaa ili kurahisisha ufuatiliaji wa kazi za wakandarasi na kuwezesha kufutilia haki za watumishi katika miradi ya ujenzi na hivyo kuleta tija katika utekelezaji wake.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Mohammed Besta amesema wamejipanga kuhakikisha usanifu unakamilika kwa wakati na taratibu za kumpata mkandarasi wa ujenzi huo unakamilika mapema iwezekanavyo.
Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amemuonya vikali Mkandaras China Railway 15 Bureau Group Corporation kutoka China anaejenga Barabara ya Mkange-Tungamaa-Pangani yenye urefu wa Km 120.8 kuhakikisha anaongeza kasi ya Ujenzi wa Barabara hiyo na Serikali haitavumilia utetezi wowote unaochelewesha ujenzi huo.
"Gharama za ucheleweshwaji wa ujenzi wa Barabara ni kubwa kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi hivyo Serikali haitavumilia mkandarasi yoyote atakayechelewesha mradi" amconya Bashungwa.
"TANROADS naendelea kuwahimiza wakandarasi na wasimamizi wa miradi ambao hawakamilishi kazi kwa kwa wakati wasipewe kazi nyingine" Amesema Bashungwa .
Barabara ya Mkange-Tungamaa -Pangani yenye urefu wa Km 120.8 ni sehemu ya Barabara kuu ya mwambao wa Afrika mashariki inayoanzia Malindi-Mombasa -Lungalunga nchini Kenya na Horohoro- Tanga- Pangani hadi Bagamoyo Makurunge yenye jumla ya km 454 ambapo kukamilika kwake kutafungua uchumi wa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment