Hayo yamesemwa na Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Katavi ACP. Kaster Ngonyani wakati akichangia mada katika Mdahalo kuhusu ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari ulioandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Katavi ambapo ameongeza kuwa jeshi la polisi limefanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji hivyo hakutakuwa na ukamataji wa wa Waandishi wa habari usiofuata sheria kama ilivyokuwa siku za nyuma
Aidha ameahidi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kusisitiza kuwa madhila yaliyowapata Waandishi wa habari wakiwa kazini huenda yalisababishwa na ukiukaji wa maadili kwa askari waliohusika katika matukio hayo
Naye SSP. Juma A. Jumanne amewataka Waandishi wa habari kuacha vitisho dhidi ya polisi ili kuimarisha mahusiano baina ya pande zote mbili.
"Tukiacha vitisho na victimization (kutuhumu) mahusiano na jeshi la polisi yataimarika" SSP. Jumanne
Mdahalo huo umefanyika jana tarehe 16.11.2023 katika ukumbi wa St. Matiasi Mpanda Mjini.
No comments:
Post a Comment