VIDEO: RUSHWA NDOGO NDOGO ZINAWAKERA WANANCHI - SIMBACHAWENE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 20, 2023

VIDEO: RUSHWA NDOGO NDOGO ZINAWAKERA WANANCHI - SIMBACHAWENE


Na Okuly Julius - Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema kuna haja ya kutengeneza sheria za kuwashughulikia viongozi walioshiriki katika masuala ya rushwa wanapostaafu ili kutoa funzo kwa viongozi wengine.


Simbachawene, amesema hayo Leo Novemba 20,2023 jijini Dodoma , wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Amesema rushwa ndogondogo bado zipo na zinawakera wananchi hivyo lazima kuwa na mikakati ya kuhakikisha zinazuiliwa.


“Kuna rushwa ambazo zinaonekana na zinaweza kuzuilika lakini kuna nyingine hazionekani hadi kufanyike uchunguzi. Lazima kutengeneza sheria ambazo zitasaidia kushughulikia viongozi walioshiriki katika masuala ya rushwa hata wanapostaafu ili kutoa somo,”alisema .


Ameongeza kuwa :”Mtu anapostaafu kama alishiriki katika uozo lazima ashughulikiwe tukifanya hivyo tutakuwa tunatoa somo kwa viongozi wengine.Tusipo shughulikiana tutakuwa hatusemi ukweli kwa Taifa letu kwasababu rushwa bado ni tatizo.


Simbachawene amesema bado yapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kuwepo kwa rushwa katika taasisi mbalimbali hali ambayo inasababisha wananchi kukosa huduma ambazo wanazihitaji.


“Bado suala la rushwa ndogondogo ni tatizo sana kwa wananchi wetu na huko ndiko yapo malalamiko mengi ya watu kutokana na rushwa hiyo kuwanyima fursa ya kupata huduma,”amesema Simbachawene


Na kuongeza kuwa :”Huduma hizo ni pamoja na elimu ngazi za chini kati hadi vyuo vikuu, lakini pia huduma za afya,kodi na leseni ambako kumewekwa utaratibu mgumu wa upatikaji wa huduma ili tuu watu watoe rushwa.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP Salum Rashid Hamduni, amesema katika mwaka wa fedha uliopita taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa sh. bilioni 171.9


Amesema fedha hizo kama zisingezuiliwa zingeishia mikononi mwa watu wasio wema ambao walikuwa na nia ya kuzifuja.


“Mafanikio tuliyoyapata katika mwaka wa fedha uliopita TAKUKURU kwa kutumia vyombo vya uchunguzi imefanikiwa kuokoa zaidi y sh.bilioni 171 fedha hizo kama zisingefuatiliwa zingeishia mikononi mwa watu na kufanyiwa ubadhilifu,”amesema


Amesema katika kipindi hicho TAKUKURU imeweza kuendesha mashitaka na sasa wapo katika asilimia 60 ya mashauri ambayo yalipeekwa mahakamani.


“Tumejielekeza zaidi kuhakikisha tunazuia rushwa na katika hili mwaka jana tulizindua TAKUKURU RAFIKI lengo ni kutanua wigo na kuwashirikisha wananchi kupata taarifa za rushwa,”alieleza


Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amempongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha uongozi imara kwa vitendo.


Amesema katika kipindi cha uongozi wa serikali ya Awamu ya Sita amendelea kuimarisha taasisi zinazosimamia haki na demokrasia ikiwemo TAKUKURU.


“Tunampongeza Rais Dk.Samia kwa kuendelea kuonyesha uongozi imara kwa vitendo ambapo amekuwa akiongeza bajeti ya taasisi hizi zinazosimamia haki na demokrasia ili zifanye kazi kwa weledi,”amesema Senyamule


No comments:

Post a Comment