WAZIRI MHAGAMA: WIZARA NA SEKTA BINAFSI ENDELEENI KUIMARISHA USIMAMIZI WA MASUALA YA DHARURA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 3, 2023

WAZIRI MHAGAMA: WIZARA NA SEKTA BINAFSI ENDELEENI KUIMARISHA USIMAMIZI WA MASUALA YA DHARURA.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama, akizungumza leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma , wakati akifungua kongamano la kitaifa la Afya Moja,lililobebwa na  Kaulimbiu isemayo:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Dkt Jim James Yonazi,akizungumza leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma , wakati wa kongamano la kitaifa la Afya Moja,lililobebwa na Kaulimbiu isemayo:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”
Sehemu ya Washiriki wa kongamano la kitaifa la Afya Moja lililofanyika Leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma,lililobebwa na Kaulimbiu isemayo:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”
Sehemu ya Washiriki wa kongamano la kitaifa la Afya Moja lililofanyika Leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma,lililobebwa na Kaulimbiu isemayo:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”
Sehemu ya Washiriki wa kongamano la kitaifa la Afya Moja lililofanyika Leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma,lililobebwa na Kaulimbiu isemayo:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”

Na Okuly Julius - Dodoma 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama ametoa wito kwa Wizara, Idara na Taasisi za Umma, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo kuendelea kuimarisha utekelezaji wa masuala ya usimamizi wa dharura ili kuhakikisha shughuli zote za maendeleo zinakuwa stahimilivu kwa maslahi mapana na Nchi.

Mhe.Mhagama ametoa kauli hiyo leo Novemba 3,2023 jijini Dodoma , wakati akifungua kongamano la kitaifa la Afya Moja ambapo amezisihi Wizara za Kisekta kuwa na mipango ya kutekeleza na kuimarisha ushirikiano wa kisekta kwa kutumia mbinu ya Afya Moja. 

Aidha,amezitaka kila sekta ishiriki kikamilifu katika tafiti kuhusu magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, utunzaji wa mazingira, usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, usalama wa chakula na lishe na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Amesama Madhara ya maafa yanayotokana na magonjwa ya milipuko ni suala mtambuka ambalo linahusu sekta nyingi na hivyo kuhitaji juhudi za pamoja katika kuweka mikakati ya kusimamia mwenendo wake kabla hayajasambaa ili kuzuia na kuimarisha mifumo ya kuyakabili pindi milipuko inapotokea ili kupunguza madhara ya maafa,hatua hii ni muhimu ili kuwa na ufanisi katika kuthibiti magonjwa ya milipuko. 

"niwahakikishie kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuzingatia na kusimamia Sera, Sheria na Mikakati kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kisekta katika kupambana na magonjwa ya milipuko na matukio yanayoathiri binadamu, wanyama na mazingira,

Na kuongeza kuwa "Serikali inaendelea kuongeza uelewa kuhusu dhana ya Afya Moja na umuhimu wake. Ni wito wangu kwa wadau wote kuungana na Serikali kuendelea kutoa elimu hasa katika ngazi ya jamii ili iweze kujilinda na magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Ni wazi jamii inapaswa kushiriki kikamilifu katika kuchukua hatua za kulinda Afya zao pamoja na wanyama na mazingira yanayowazunguka. ," amesisitiza Mhagama

Mhagama amesema ,Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu imeendelea kuimarisha mifumo ya utendaji ya usimamizi wa maafa yanayoathiri afya ya binadamu, wanyama, mimea na mifumo ya ikolojia kupitia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Mwaka 2004 ambayo imeweka kipaumbele udhibiti wa magonjwa ya milipuko ili kuzuia maafa yanayoweza kutokea. 

Aidha, Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na.6 ya Mwaka 2022 inabainisha majukumu ya kutekelezwa kwa kuzingatia ushirikiano wa wadau kwa dhana ya afya moja. Vilevile, Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa 2022 – 2027 umeanisha umuhimu wa kutekeleza hatua za kuimarisha uwezo wa kutumia dhana ya afya moja kwa maafa yanayohusiana na masuala ya afya katika ngazi zote kwa ustahimilivu wa jamii. 

"Dhana hii ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya sekta zinazohusika na afya ya binadamu, wanyama na mazingira kwa ajili ya uratibu na usimamizi katika utendaji na kupanga mikakati ya pamoja inayolenga kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na milipuko ya magonjwa na visumbufu vya mimea na mazao ikiwemo madhara ya majanga yanayovuka mipaka na yanayoweza kusambaa kwa muda mfupi, usugu wa vimelea dhidi ya dawa, usalama wa chakula na lishe na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,"amesema Mhagama.

Nao baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wamesema kuwa dhana ya Afya moja faida yake ni njia inayowaleta pamoja na sekta mbalimbali ambapo ni afya, mifugo na wanyamapori ili kukabiliana na changamoto zinazohusiana na afya.

“Upande wa kutumia afya moja maana yake tumefanikiwa kuhakikisha kwenye masuala yanayohusiana na milipuko ya magonjwa tunaenda kama sekta mbalimbali tunaziratibu sekata na kuzisimamia kwamba zinasaidia kutatua changamoto ya afya kwa wakati mmoja,”wamesema.


Kaulimbiu ya kongamano hili inasema:-“Afya Moja: Mbinu ya Pamoja kuboresha afya ya binadamu, wanyama, mimea na mfumo wa ikolojia kwa ustahimilivu wa maafa.”

No comments:

Post a Comment