Kamanda wa Kikosi Cha Cha Usalama Barabarani Tanzania SACP Ramadhani Ng'anzi amewapongeza madereva wanaoendesha malori yanayobeba makaa ya mawe kutoka Kitai Amani mkoa wa Ruvuma kwenda Mikoa ya Dar es Salaam, Mbaye, Tanga, Mtwara na pia wanaopeleka nje ya nchi kama Uganda na Kenya.
Pamoja na pongezi hizo alizozitoa Kamanda amewataka waendelee na moyo wa kuepusha ajali hata kama kuna dereva mwingine anataka kusababisha ajali, wajaribu kuwa na udereva wa kujihami popote inapotokea kama kuna uzembe wa madereva wengine.
Kamanda amewataka madereva hawa kujiendeleza kusoma upya kwani magari ya sasa ni mapya na mifumo ni mipya kwa hivyo wajitahidi kwenda upya darasani.
Kamanda wa Kikosi amewataka madereva wote wahakiki leseni zao kwa lengo la kuwajua madereva wanapokuwa barabarani.
Hivyo amewahimiza madereva wahakiki ili kuepusha usumbufu unaojitokeza wakati wa ukaguzi wa madereva ambao hawajahakiki leseni zao.
Halikadhalika, amewataka waendelee kutii sheria za usalama barabarani ili waweze kuepusha ajali za barabarani.
Pia, kamanda amewataka waache kuendesha malori kwa mwendo kasi na kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari,wasiendeshe malori wakiwa wametumia aina yeyote ya kilevi.
Na mwisho amewatakia maandalizi mema ya sikukuu ya Christimass na mwaka mpya.
No comments:
Post a Comment