Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania SACP Ramadhani Nga'anzi ametoa onyo kwa Magari mabovu kutokanyaga Barabarani.
SACP Ng'anzi ametoa onyo hilo Disemba 22,2023 akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Mtwara, wilaya ya Masasi.
Katika wilaya hiyo amekagua mabasi yapatayo 15 na kati ya hayo basi 1 lilibainika kuwa ni bovu halifai kuendelea na safari, kwani lilikuwa na hitilafu kwenye mfumo wa break.
Kamanda amedhamiria kudhibiti ajali kwa kushirikiana na wadau wengine wa usalama barabarani wakiwemo RSA, LATRA, TIRA, TRA na TANROAD.
Kamanda Ng'anzi anasikitishwa sana na kuumizwa sana na ajali za barabarani zinapotokea na kupelekea vifo, majeruhi na uharibifu wa miundo. Kamanda amesema hafurahishwi kuona madereva wanaendesha magari yao yakiwa hayajakaguliwa na wakati wana mafundi wao binafsi.
Kamanda amesikitika sana kuona ajali zinazotokea kwa sababu ya gari kukosa mfumo wa breki , amewataka wamiliki wote wa magari kutumia mafundi wao binafsi kutengeneza magari kabla ya kuliingiza barabara kwani Jeshi la polisi litafanya ukaguzi wa kina ili kuyabaini magari mabovu na kutoyaruhusu kufanya shughuli za usafiri na usafishaji.
Kamanda amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mmiliki na dereva yeyote atakaeruhusu gari lake kutumika barabarani likiwa bovu.
SACP Ng'anzi amesema ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza basi anawataka wamiliki na madereva kuhakikisha wanatengeneza magari yao.
No comments:
Post a Comment