MATUKIO KATIKA PICHA : DKT.SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU NA UZINDUZI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Saturday, December 9, 2023

MATUKIO KATIKA PICHA : DKT.SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 62 YA UHURU NA UZINDUZI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru kuhusu kazi mbalimbali ambazo zinafanyika katika Tume hiyo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2023. Maadhimisho hayo pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, yamefanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Msajili wa Hazina Bw. Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili katika Banda la Maonesho la Hazina wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2023 pamoja na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru pamoja Makamishna wa Tume ya Mipango wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw. Lawrence Mafuru pamoja na baadhi ya Watumishi wa Tume hiyo na Wajumbe wa Bodi wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 9 Desemba, 2023.

No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

BIL 97.178 KUTUMIKA UJENZI BARABARA YA IFAKARA-MBINGU

Imeelezwa kuwa mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ifakara hadi Mbingu yenye urefu wa kilomita 62.5 utatumia Bilioni 97....