MHE. MWANAIDI ATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUKAMILISHA MFUMO WA USTAWI WA JAMII. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, December 14, 2023

MHE. MWANAIDI ATAKA WADAU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUKAMILISHA MFUMO WA USTAWI WA JAMII.


Na WMJJWM, Dar Es Salaam

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ametoa wito kwa wadau wa Ustawi wa Jamii kushirikiana na serikali kutekeleza Mpango wa Bajeti ya uundaji wa Mfumo wa Ustawi wa Jamii (Comprehensive Social Welfare System).


Mhe. Mwanaidi ametoa wito huo Desemba 13, 2023 wakati akizindua Wiki ya Huduma za Ustawi wa Jamii sambamba na Maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Ustawi Jamii kwenye eneoa Mnazi mmoja nijini Dar Es Salaam.


Amewataka pia wadau kushiriki na kuwekeza rasilimali kwenye mchakato wa kukamilisha uundaji wa Sheria ya Wataalamu wanaotoa Huduma za Ustawi wa Jamii nchini, kuwekeza rasilimali katika mchakato wa mapitio ya Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 na , uendelezaji wa Vituo vya kulea Watoto Wadogo Mchana.

"Toeni huduma kwa kuzingatia Sera, Sheria, Miongozo, Kanuni na vipaumbele vya Serikali,
Wadau wote wajiunge kwenye Vikosi kazi vilivyoundwa na Wizara kwa lengo la kujadili namna bora ya kuimarisha na kuendeleza huduma za Ustawi wa Jamii katika maeneo mbalimbali ya nchi" amesisitiza Mwanaidi.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana wa chuo cha Ustawi wa Jamii Mhe. Sophia Simba amesema chuo kimeendelea kutoa huduma za jamii, ikiwepo Msaada wa Kisaikolojia na namna bora ya kukabiliana na afya ya akili pamoja na elimu kuhusu Usuluhishi wa Migogoro ya ndoa.

Mhe. Sophia ameiasa Jamii kuwatumia wataalamu wa Ustawi wa Jamii kwenye shughuli mbalimbali akieleza kuwa Maendeleo ya Taifa lolote yanategemea Afya na Utimamu wa Akili na kutolea mfano wa shughuli hizo ni kuwasaidia kisakolojia wananchi waliohamishiwa kijiji cha Msomera pamoja na waathirika wa mfuriko wilaya ya Hanang' hivi karibuni.

Akizungumza kwa niaba ya wataalamu wa Ustawi wa Jamii Afisa Ustawi wa Jamii ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Elisha Nyamara ameishukuru Wizara na Ofisi Rais-TAMISEMI kwa kuwa na Wiki ya Ustawi ambayo inatoa wigo wa Wataalam lakini pia wananchi wanapata huduma.

"Mkoa wa Dar Es Salaam ambao una wananchi zaidi ya milioni 5. Kwetu hii ni fursa adhimu na tunaahidi kuhakikisha wananchi wanajitokeza kwa wingi." amesema Nyamara.

No comments:

Post a Comment