Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,SACP. Ramadhani Ng'anzi akiwa katika Ziara ya kikazi Mikoani amepiga tochi Magari na kukamata Madereva wanaoendesha Kwa Mwendokasi barabarani.
Kamanda ameyafanya hayo Disemba 21,2023 akiwa barabarani mkoa wa Kipolisi WA Rufiji kwa ajili ya kupambana na madereva wanaoendesha magari yao kwa mwendokasi barabarani licha ya kuwa mazingira barabara yanaonyesha kuna Shule, Hospital na makazi ya watu.
Katika operesheni yake amefanikiwa kuwakamata baadhi ya madereva wakiwa wanaendesha mwendokasi katika maeneo ya shule na kuna ukomo wa mwendo kasi kinaelekeza kilomita 50 kwa saa.
Miongoni mwa madereva waliokamatwa kwa mwendo kasi walikuwa wanadaiwa madeni kati ya Tshs 60,000/- na 37,500/.
Wadaiwa wote hawa waliamuriwa kulipa fedha hizo wanazodaiwa ndipo waendelee na safari zao.
Kamanda amewaonya watendaji wanaotumia speed Camera kutotumia kifaa hicho kuwabambika madereva makosa ya mwendokasi yanayopelekea malalamiko mengi yanayolichafua Jeshi la polisi.
Amewaelekeza askari hawa kuwa na kitabu cha kuandika magari wanayoyakamata na hatua wanazochukua na wawe wanatuma taarifa ya ukamataji wa kila siku.
No comments:
Post a Comment