Disemba 21,2023 Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani , SACP. Ramadhan Nga'nzi akiwa katika ziara ya kikazi mkoa wa Lindi amekagua vifaa vya Jeshi la Polisi ambavyo ni POS MACHINE ya kuandikia notification ya makosa ya usalama barabarani.
Katika ukaguzi wake alimkamata dereva aliyekuwa amefanya kosa la barabarani. Na aliamuru aandikiwe faini kwa kosa alilolifanya.
Baada ya zoezi hilo kukamilika alimwambia dereva husika kuwa akalipe faini hiyo kwa wakati ili deni lisizidi , kwani deni likizidi atakamatwa na vifaa vya Jeshi la polisi vilivyosambazwa barabarani nchi nzima kwa ajili ya kukamata wadaiwa sugu.
SACP Ng'anzi ametoa wito kwa wananchi wote kukagua wenyewe magari yao kama wanadaiwa kwa kutumia mfumo huu wa tms.tpf.go.tz kwa kuandika kwenye Google halafu atajaza namba ya gari na mwisho mfumo utamwambia kuwa gari inadaiwa au haidaiwi.
Pia amewataka wananchi kulipa madeni wanayodaiwa kwani wakikamatwa na mfumo inabidi wasimamishwe hadi walipe deni lote wanalodaiwa.
Halikadhalika, amekagua mfumo wa ufuatiliaji na ukamataji wa madeni yatokanayo na tozo za makosa ya barabarani ambapo amebaini kuwa upo sawa na unafanya kazi.
No comments:
Post a Comment