VILIO MGAO WA UMEME MWISHO 2024 - MRAMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 20, 2023

VILIO MGAO WA UMEME MWISHO 2024 - MRAMBA

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera ,Disemba 20,2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera ,Disemba 20,2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Gissima Nyamo-Hanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera ,Disemba 20,2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Gissima Nyamo-Hanga,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera ,Disemba 20,2023.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera, Moses Holela ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi wa kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera ukaguzi uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,Mhandisi Felchesmi Mramba na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Gissima Nyamo-HangaDisemba 20,2023.
Muonekano wa Kiwango Cha Maji katika Bwawa la Mtera .


Na Okuly Julius-Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, amesema mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere utaanza majaribio Januari 16, 2024 ambao utaongeza Megawati 235 kwenye gridi ya Taifa na kuongeza kiasi cha umeme.


Maramba, ameyasema hayo Leo Disemba 20,2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwango cha maji katika chanzo cha kuzalisha umeme cha Bwawa la Mtera.


“Hivi sasa kweli hali ni mbaya ya umeme nchini kutokana na vyanzo vyetu tunavyovitegemea kuzalisha umeme ikiwemo hichi cha Mtera kukosa maji licha ya uwepo wa mvua katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Lakini mvua hizi ambazo zinanyesha hivi sasa nyingi ni za mikoa ya kanda ya Pwani na Ziwa Vickitoria hivyo vyanzo vyetu vya Mtera na Kidatu havipati maji ya mvua hizo”amesema Mramba

Aidha, Mramba amesema, kutokana mvua ambazo zinatarajiwa kuanza kunyesha kati ya Desemba 25 na 26 mwaka huu zitasaidia kuongeza maji katika vyanzo hivyo ambavyo vinategemea maji kutoka mikoa ya Iringa, Mbeya, Tabora, Singida na Dodoma.

“Lakini pia mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere utaanza majaribio Januari 16, 2024 ambao utaongeza Megawati 235 kwenye gridi ya Taifa na kuongeza kiasi cha umeme”amesema

Kadhalika, amesema mtambo wa pili utaanza majaribio mwezi Machi na kuongeza Megawati zingine 235 na kufanya mgao wa umeme kuisha kabisa nchini.

“Niwahakikishie Watanzania kweli hivi sasa tunanjaa lakini chakula kipo jirani kabisa kwani katika kipindi hichi kuanzia wiki ya tatu ya mwezi Januari 2024 hadi mwezi Machi tatizo la mgao litakuwa limekwisha kabisa nchini”amesema

Katibu Mkuu huyo amesema pamoja na kusubiri mvua kuanza kunyesha na majaribio ya mitambo ya kuzalisha umeme katika bwawa la Mwalimu Julius Nyerere wanaendelea na jitihada za kufanyia kazi malalamiko ikiwemo kupunguza makali ya umeme.

“Hivi sasa kunamalalamiko mengi kwa wananchi kuhusu mgao mkali wa umeme katika baadhi ya maeneo na maeneo mengine kupendelewa”aliongeza

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),Gissima Nyamo-Hanga amesema mgao wa umeme unaoendelea unazingatia mahitaji na kusisitiza kuwa Shirika lake limekuwa likisimamia kwa umakini mgao huo.


"Mkakati wetu ni kuhakikisha mgao unakuwa sio wa kuuliza na umeme unarejeshwa kwenye maeneo ya mgao kwa muda uliopangwa."

Aidha, Nyamo-Hanga amesema mvua zinazonyesha ukanda wa Pwani na wa Ziwa hatoi majibu katika kuzalisha umeme katika vituo vya Mtera na Kidatu.


" Mvua za Pwani zinapeleka maji Bahari ya Hindi na vituo vya Mtera na Kidatu vinategemea mvua ambazo zinazonyesha Mikoa ya Iringa na Mbeya inayojaza Mito ya Ruaha Mkubwa na Ruaha Mdogo wakati Mto wa Kizigo unajanzwa na mvua za Tabora, Singida na Dodoma.


Naye Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa TANESCO, Aloyce Simon amesema kwa sasa Bwawa la Mtera linazalisha megawati 40 chini ya uwezo wake wa kuzalisha megawati 80.


" Maji haya yakizalisha umeme hapa yanaenda kuzalisha umeme katika kituo chetu cha Kidatu, hivyo kutokana na hali ya maji kuwa kina cha chini linazalisha megawati 40 yanaenda Kidatu na kuzalisha megawati 60 chini ya uwezo wa kituo hicho ya kuzalisha megawati 200."amesema Simon


Awali, Kaimu Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera, Moses Holela amesema baada ya mvua kidogo kunyesha Kanda ya kati Bwawa limefikia kina cha chini cha mita za ujazo 690.4 juu ya usawa wa bahari ambapo kiwango cha wastani ni mita za ujazo 698.5 juu ya usawa wa bahari.

No comments:

Post a Comment