DKT. TULIA AHIMIZA MAZOEZI KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU MAGONJWA YASIYOKUWA YA KUAMBUKIZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 27, 2024

DKT. TULIA AHIMIZA MAZOEZI KUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU MAGONJWA YASIYOKUWA YA KUAMBUKIZA


Na Carlos Claudio DODOMA 

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amehimiza wananchi kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ili kupunguzia taifa mzigo wa kufanya matibabu kwa magonjwa yasiyo ambukiza ambayo yanaepukika kwa kushughulisha mwili.

Dkt. Tulia Ackson amesema hayo leo Januari 27,2024 katika Bonanza la Wabunge wanaoshabikia timu ya Yanga na Wabunge wanaoshabikia timu ya Simba katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.

Amesema zoezi la haya mabonanza yamechukua sehemu kubwa mawazo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo akiwa Makamu wa RAIS aliyeanzisha mazoezi ambayo nchi nzima walipaswa kufanya mazoezi kila baada ya wiki mbili.


“Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kama wawakilishi wa wananchi wa Tanzania basi tumechukua hilo kwa uzito mkubwa kabisa ndio maana huwa tunafanya mabonanza kila bunge linapokutana nia ya kufanya mabonanza haya pamoja na kwamba tunafanya mazoezi ili sisi tuwe na afya ya kuwatumikia waliotuchagua vizuri lakini tunafanya pia mazoezi kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kuendeleza utamaduni ambao Dkt. Samia Suluhu Hassan alituwekea msingi mzuri alipokuwa Makamu wa Rais.”

Na kuongeza kuwa “Sisi kama taifa tufike mahali ambapo watu watazoea kufanya mazoezi na hivyo kupunguzia taifa letu mzigo wa kufanya matibabu yenye magonjwa yasiyo ambukiza ambayo kwa kuushugulisha tu mwili tumeweza kuepukana nayo na sisi kama Bunge tunajaribu kufanya tathmini kwa sasa ili tuone kwa namna gani haya mabonanza yametusaidia kupunguza fedha tunazozitumia kwenye matibabu ya Waheshimiwa wa Bunge”.amesema Mhe. Ackson.

Mhe. Ackson aliendelea kusema mabonanza ya wabunge huwa yanafanywa kila Bunge linapokaa na anatoa pongezi kwa Azania Bank kudhamini Bunge Bonanza ya mwaka 2024 kuwa ya maboresho na utofauti wa michezo iliyoleta ushindani kutoka kwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Mhe. Ackson ameeleza Bunge inategemea kufanya Bunge Marathon ambayo itakuwa tofauti na mabonanza kwasababu dhamira ya kuanzisha Bunge Marathon ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya elimu nchini kwani wameshawahi kujenga shule ya sekondari ya wasichana mkoani Dodoma ya Bunge Girls Secondary School na makusudio yao ni kujenga shule ya secondari ya watoto wa kiume na kupitia Bunge Marathon itakayofanyika mwezi wa 4,2024 itakuwa na makusudio hayo hivyo kuendelea kuhamasisha wadau kujitokeza na kujiandikisha kwa shilingi elfu 40 na kupata vifaa vya kukimbilia.

Azania Bunge Bonanza 2024 lenye kauli mbiu ‘Utani wetu ni Umoja wetu’ ilikuwa na idadi ya michezo ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, kukimbiza kuku, uvutaji wa kamba na michezo kadhalika na kwa upande wa mpira wa miguu wabunge mashabiki wa Yanga wameendeleza ubabe dhidi ya wabunge mashabiki wa Simba mara baada dakika 90 za mchezo huo kumalizika kwa sare 1-1 na ikalazimu mikwaju ya penati kupigwa huku timu ya Yanga iliibuka na ushindi.


No comments:

Post a Comment