NAIBU WAZIRI SILINDE AWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA YA BBT KUBORESHA KILIMO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 27, 2024

NAIBU WAZIRI SILINDE AWATAKA VIJANA KUTUMIA FURSA YA BBT KUBORESHA KILIMO


Na Renatha Msungu DODOMA

NAIBU Waziri wa Kilimo David Silinde amewataka vijana kutumia nafasi waliopewa ili kuionesha jamii kuwa wanaweza kufanya Kilimo.

Silinde amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya vijana wa Jenga Kesho iliobora BBT.

Amesema vijana hawa ambao ni awamu ya kwanza wanapaswa kufanya jitihada katika kuhakikisha wanafanya vizuri katika Kilimo wanachokwenda kulima.

Amesema katika eneo hilo la Chinangali wanakwenda kulima alizeti ambayo itakwenda kununuliwa kwa ajili ya kuzalishaafuta.

Akizungumzia kuhusu soko la zao hilo Naibu Waziri amesema linakwenda kununuliwa na serikali hivyo vijana hao wasiqe na wasiwasi.

Silinde amesema serikali imejipanga kuhakikisha wanafanikiwa katika Kilimo hiko ili vijana waweze kujiinua kiuchumi.

Naye Rehema Menda Mrakibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji amesema wameamua kutoa Mafunzo ya Sayansi ya moto aina mbalimbali ya Moto pamoja na kujua mbinu za uzimaji Moto.

Amesema wamefanya hivyo ili waweze kuchukua tahadhari dhidi ya moto au vyanzo navyo vinaweza kuleta athari katika Makazi yao.

Amesema wanafundisha pia namna ya kutumia kemiko mbalimbali pamoja na matumizi ya mbolea na utunzaji wa mbolea ili kuepuka na majanga ya moto.

No comments:

Post a Comment