POLISI FAMILY DAY IKAWE CHACHU YA UTENDAJI KAZI KWA JESHI LA POLISI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 27, 2024

POLISI FAMILY DAY IKAWE CHACHU YA UTENDAJI KAZI KWA JESHI LA POLISI DODOMA


"Kuwepo kwa siku hii adhimu ya Polisi Family Day ni furaha na ni faraja hivyo ni wapongeze kwa hili na muendelee kufanya kazi kwa weledi na kulinda heshima ya Jeshi la Polisi"

Kauli hiyo imetolewa Januari 27, 2024 na Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Jabir Shekimweri wakati akizungumza na Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbali mbali pamoja na wanafamilia wa askari polisi katika sherehe ya Polisi Dodoma ( Police Family Day) iliyofanyika katika viwanja vya kilimani jijini Dodoma.

Aidha, Shekimwery amewataka askari Polisi kuendeleza siku hii na kusisitiza kukuza vipaji vilivyopo katika familia ya Askari Polisi ambao wameshiriki katika michezo mbali mbali na kuonesha vipaji walivyo navyo.

Katika sherehe hiyo michezo mbalimbali imefanyika iliyo shirikisha Askari Polisi, wanafamilia pamoja na wananchi.

Toka dawati la Habari Dodoma

No comments:

Post a Comment