Na Okuly Julius-Dodoma
Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea Vifaa hivyo Leo Februari 20,2024 Jijini Dodoma,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Mwinyikondo Juma Amir amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kutunza na kutumia Vifaa hivyo kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Pia amesema kuwa Wizara ya Afya inatambua Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) kama kitivo au Chanzo Cha huduma za uchujaji wa Damu kwa watu walioathirika na maradhi ya Figo hususani katika ukanda huu wa kati.
"Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) inatambulika Kwa kuwa kitivo au Chanzo Cha huduma za uchujaji wa Damu kwa wenzetu wenye maradhi ya Figo na ukweli ndio kilikuwa kitua Cha kwanza ambacho kilifunguliwa rasmi Mwaka 2013 kwa ukanda huu wa kati na Wizara yetu ya Afya inalitambua hilo,"amesema Dkt. Mwinyikondo
Pia ameipongeza Taasisi ya "AL NMAA SOCIETY" kwa msaada huo huku akibainisha kuwa Taasisi hiyo imeiongezea nguvu Serikali ya kuhudumia Wananchi wake kwani kwa vifaa tiba na vitendanishi hivyo idadi ya wananchi watakaohudumiwa katika hospitali hiyo itaongezeka.
Amesema suala la vifaa ni moja ya chagizo la kuongeza utoaji wa huduma bora hivyo ametoa wito kwa Taasisi zingine kujitokeza na kutoa misaada mbalimbali sio tu kwa Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ila Kwa hospitali zote nchini ili kuboresha utoaji huduma.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM Prof. Lughano Kusiluka amesema vifaa tiba na vitendanishi hivyo vitasaidia kuondoa changamoto na mapungufu mbalimbali yaliyokuwepo katika Hospitali hiyo na huduma zitakuwa zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.
Pia ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuipandisha hospitali hiyo kuwa ya ngazi ya Wilaya na hiyo inaonyesha imani ya Serikali kwa hospitali hiyo na ahadi yao ni kuendelea kutoa huduma Bora sio kwa wanachuo tu hata kwa Wananchi kwa ujumla.
"Wadau hawa ni muhimu sana kwetu na kwa taifa kwa ujumla kwani wanaifanya Tanzania kuwa sehemu salama na Wananchi wake kuwa na Afya njema hivyo ni vyema sisi kama Chuo Kikuu Cha Dodoma tiwashukuru na kuthamini msaada huu waliotupatia kwani inakwenda kuwa chachu katika utendaji wa watumishi wetu katika Hospitali hii,"ameeleza Kusiluka
No comments:
Post a Comment