LAMBERT : "MAKONDA ANAFANYA KAZI NI KAMA HUKO AWALI SERIKALI HAIKUWEPO" - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 14, 2024

LAMBERT : "MAKONDA ANAFANYA KAZI NI KAMA HUKO AWALI SERIKALI HAIKUWEPO"


MBUNGE wa Viti Maalum Agnester Lambert jana Februari 13 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) amesema ziara ya Katibu wa Itikadi Siasa Uenezi na Mafunzo Paul Makonda inaonesha kuwa ni kama huko awali Serikali haikuwepo.

Amesema katika Ziara ya Mwenezi huyo Makonda badala ya kwenda kueleza namna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametekeleza kwa namna gani Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM )amejikuta hafanyi hayo bali ana sikiliza na kutatua kero za wananchi.

"Mhe.Mwenyekiti natambua Wakuu wa Mikoa ndio wasimamizi namba moja wa shughuli za Serikali kule chini, ndio wasimamizi namba moja wa fedha za Serikali na maendeleo zinazoshushwa kule chini na wote tunatambua kama jinsi ilivyo mbunge ana jimbo lake la uchaguzi ndivyo ilivyo kwa Wakuu wa Mikoa nao wana majimbo yao kule chini ambayo ndio Mikoa,

"Ni jimbo la uteuzi ambalo Mhe.Rais amemteua ameuamini ,tofauti na yale mema na mazuri yaliyofanywa na Mhe.Rais yanapaswa kusikika kule chini Wakuu wa mikoa hawa wakuu wa wilaya wakurugenzi wameshindwa kabisa kutekeleza wajibu wao kabisa kwa asilimia 100 Mhe.Mwenyekiti" amesema Lambert 

Amesema katika mikoa yote aliyokwemda Mwenezi huyo Makonda inafika sehemu anazuia kuongozana na wateule hao wa Rais akisema wabaki washughulikie kero za wananchi.

"Mfano Katika ziara ya Mkoa wa Rukwa aliwahi muambia Mkurugenzi kwamba sikuruhusu uambatane na mimi na kuacha hapa katika Halmashauri yako utatue changamoto hizi na katika ziara yake anawaweka wote Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Mkoa Wakurugenzi kesi inaisha pale pale"

Lambert amesema hiyo ni hujuma ya moja kwa moja kwa Mhe. Rais kwani ikiwa Mkuu wa Mkoa Mkurugenzi, Mkuu wa Wilaya wakisimama vizuri kumsaidia Rais Kazi hakutakuwa na changamoto ya miaka kumi wala mitano.

No comments:

Post a Comment