MATUKIO KATIKA PICHA NYUMBANI KWA HAYATI LOWASSA KIJIJI CHA NGARASH WILAYA YA MONDULI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 15, 2024

MATUKIO KATIKA PICHA NYUMBANI KWA HAYATI LOWASSA KIJIJI CHA NGARASH WILAYA YA MONDULI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiwafariji watoto wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Kijiji cha Ngarash Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha tarehe 15 Februari, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Rombo Mhe. Joseph Selasini kwenye Msiba wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Kijiji cha Ngarash Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akizungumza na Makatibu Wakuu kwenye msiba wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, msibani katika Kijiji cha Ngarash Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Anderson Mutatembwa katika Msiba wa Hayati Edward Ngoyai Lowassa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake katika Kijiji cha Ngarash Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment