ZOEZI LA UTAFITI WA GHARAMA ZA UTAPIAMLO LAZINDULIWA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 14, 2024

ZOEZI LA UTAFITI WA GHARAMA ZA UTAPIAMLO LAZINDULIWA DODOMA


Na Okuly Julius - Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera,Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga amesema tafiti zinazofanyika nchini ni moja ya jitihada za kutafuta shahidi za kisayansi zinazoweza kuisaidia Serikali kuboresha harakati zake za kuondokana na athari za utapiamlo (hasa udumavu kwa watoto pamoja na uzito uliozidi au kiribatumbo kwa watu wenye miaka 15-49).


Naibu Waziri Ummy ametoa kauli hiyo Leo Februari 14,2024 jijini Dodoma, wakati akizindua rasmi zoezi la utafiti wa gharama za utapiamlo hapa nchini ,kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama.


Ambapo amesema lengo la utafuti huo ni kupata taarifa sahihi zitakazochagiza harakati za kuelekea maendeleo endelevu na kuimarisha ustawi wa Taifa kwa kupitia nguvukazi ya watu wenye afya njema, ufahamu mzuri na wenye uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.


"Ni jukumu letu sote kama Serikali na wadau kuhakikisha tunafanya tafiti nyingi zinazogusa changamoto zilizo katika jamii zetu na tafiti hizo zitatusaidia kuimarisha ustawi wa Taifa letu kupitia nguvukazi ya watu wenye afya njema, ufahamu mzuri na wenye uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kiuchumi," ameeleza Naibu Waziri Ummy

Na kuongeza kuwa "Lengo la utafiti ni kubainisha makadirio ya gharama zinazosababishwa na matatizo ya lishe duni/utapiamlo; kijamii na kiuchumi na hususan katika nyanja za sekta ya afya, elimu na nguvu kazi.


Amesema Tanzania itakuwa nchi ya 22 barani Afrika kufanya utafiti kama huu pindi utakapokamilika.


Kwa mwaka 2024, takribani nchi 6 za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania, Namibia, Cote’divore, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Somalia , zimeonesha utayari wa kufanya utafiti huo ili kuwezesha nchi kupanga malengo ya kupunguza upotevu wa pato ghafi itokanayo na utapiamlo na kuwekeza katika maeneo ya maendeleo.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka UNICEF Bw. John George ametoa pongezi kwa Serikali kwa kujiunga na Mpango wa COHA na kutambua nafasi ya mtoto ambaye ndiye mlengwa mkubwa katika mpango huo na kwa tafiti zilizotoa takwimu za utapiamlo nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwakilishi Mkazi Nchini, wa Progamu ya Chakula Duniani (WFP) Bi Sarah Gibson Alisema Tafiti hizo zitasaidia kukabiliana na madhara yatokanayo na Utapiamlo nchini kama vile ukuaji kwa mtoto na huweza kuleta athari katika elimu ya mtoto na Maendeleo ya Taifa kwa Ujumla.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw.Salihina Ameir alisema kwa Upande wa Zanzibar, Ofisi hiyo ina nafasi kubwa katika Uratibu wa masuala ya Kiuchumi kisiasa na Kijamii ikiwa ni Pamoja na masula ya Tafiti za Lishe.

Zoezi hili la suala zima la uzinduzi wa gharama za zoezi la Tafiti za Utapiamlo nchini, linafadhiliwa na Programu ya Chakula Duniani (WFP) pamoja na wadau wengine wa maendeleo nchini kama vile USAID, FAO, Irish Embassy, Hellen Keller International – HKI na UNICEF

Utafuti huo ni utekelezaji wa maazimio ya viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kupitia mpango ujulikanao kama “The Cost of Hunger Study in Africa – COHA” ambapo Mheshimiwa DKt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameridhia ufanyike.

No comments:

Post a Comment