SERIKALI IMETIMIZA MAJUKUMU YAKE KATIKA SEKTA YA AFYA- MHE. UMMY MWALIMU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 15, 2024

SERIKALI IMETIMIZA MAJUKUMU YAKE KATIKA SEKTA YA AFYA- MHE. UMMY MWALIMU.


Na Carlos Claudio, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweza kutimizia majukumu yake katika sekta ya afya hivyo kubakisha jukukumu la waganga Wafawidhi kwenda kutimiza majukumu yao katika kuhudumia wananchi.

Pia imewatangazia waganga wafawidhi kuwa kwasasa hawatokagua suala la huduma tu wanazozitoa bali wataingia mpaka kwenye upande wa vipimo vya maabara ili kuweza kusaidia utoaji wa huduma bora unaendelea kuimarika.

Akizungumza  February 14,2024 Jijini Dodoma Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya Msingi na kuongeza kuwa kadri huduma zinavyozidi kupanuliwa katika maeneo yote nchini ndivyo wahitaji wanazidi kuongezeka.

“Nataka niwashukuru sana kwani mnafanya vizuri katika maeneo yenu licha ya changamoto mbalimbali mnazozipitia ndiyo maana kila siku naendelea kuwa mtetezi wenu, unakuta ninyi mmekuja hapa lakini kuna kituo kimefungwa mtoa huduma wao kaja hapa kwakweli niwapongeze sana kwa namna mnavyojitoa,”amesema Mwalimu.

Amesema pia waganga wafawidhi wahakikishe huduma zinazotolewa katika vituo vya afya zinazigatia ustawi wa jamii kwa kuanzisha dirisha la kuhudumia wazee pamoja na kuweka takwimu za wagonjwa wanaotumia huduma za msamaha zinarekodiwa.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Wilson Mahera amemuomba Waziri Ummy mwongozo wa uchangiaji wa bima za afya ukamilike kwa wakati ili kuwasaidia watumiaji wa huduma hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI na Rashidi Mfaume amesema kuwa waliamua kufanya mkutano huo kwasababu kumekuwa na nafasi kubwa ya mawasiliano na kushindwa kupata marejesho wa kiutendaji kutoka kwao baadala yake kupata kutoka kwa vyombo vya habari na wananchi.

“Tumekuwa na uwekezaji mkubwa kuanzia ngazi ya msingi kwenye upande wa dawa na vifaa tiba na sasa Rais hatumdai bali yeye anatudai na ni fursa kwao waganga hawa kubadiliashana uzoefu katika utendaji wao wa kazi,”amesema.

Amesema kuwa moja kati ya malengo makubwa ya mkutano huo ni kuwajengeana uwezo katika nafasi mbalimbali za utendaji kazi ikiwemo kupata taarifa kuhusiana na afua mbalimbali zinazoendeshwa na na Serikali na hali ya ufuatiliaji utendaji wa kazi unaofanywa na TAMISEMI.

“Pia kupitia mkusanyiko huu tumepata maoni mbalimbali na tunaahidi kwenda kuyafanyia kazi maoni yao ambayo wameyawasilisha ndani ya siku hizi mbili tulizokutana nao hapa.

Akisoma risala kuhusiana na hali ya utendaji kazi mbele ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi Dkt. Florence Hilary ameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini ikiwemo kununua vifaa tiba, ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo ya karibu na wananchi.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kufunga mifumo ya kielektroniki katika vituo mbalimbali vya afya jambo ambalo limeelekea kukabiliana na upotevu wa fedha uliokuwepo hapo awali na hiyo kusaidia ongezeko la ukusanyaji wa mapato kupitia sekta ya afya.

“Tunaipongeza Serikali kwa kuendelea kusimamia vyema sera ya afya ya mwaka 2007 na kutekeleza vyema ilani ya chama katika kuendelea kuboresha huduma za afya nchini,”amesema.

Aidha ameongeza kuwa lengo la uanzishwaji wa maduka ya madawa ni kurahisisha upatikanaji wa dawa kwa urahisi kwa wagonjwa lakini changamoto inakuwa ni pale ambapo mgonjwa anayetibiwa kwa msamaha akitakiwa kulipia dawa hizo.






No comments:

Post a Comment