Na. Asila Twaha, Moshi
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais -TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde ametoa wito kwa walimu kuendelea kufanya kazi na kutokukatishwa tamaa na baadhi ya watu akiwaeleza Serikali itaendelea kuhakikisha haki na hadhi ya walimu inalindwa.
Haya ameyasema katika kikao alicho kaa na walimu wa shule za sekondari na msingi wa Halmashauri ya Wilaya Moshi tarehe 19 Machi, 2024 katika shule ya sekonadari weru weru Mkoani Kilimanjaro.
“ninyi ni wasaidizi wa Mhe. Rais katika eneo la elimu na anawaamini sana nitoe wito fanyeni kazi kukisaidia kizazi cha Tanzania” amesema Dkt. Msonde
Dkt. Msonde amesema Serikali imeendelea kushughulikia changamoto za walimu zikiwemo kupandishwa madaraja, kubadilishwa kwa muundo (recategorization), madai ya uhamisho, malipo ya pesa za likizo, malimbikizo ya mshahara, na kuwashugulikia wale wote wanatoa kauli zisizoridhisha kwa watu wanaowahudumia walimu.
Amesema changamoto hizo zimeendelea shughulikiwa na kuhusu kupandishwa kwa madaraja maafisa utumishi wa mikoa na halmashauri walishapitia kwa kila mtumishi mwalimu mmoja mmjoja na walimu wapatao 278,000 tayari taarifa zao zipo ili kila mtu apate haki yake.
Aidha, amesema tayari kazi hiyo imeshafanyika chini ya usimamizi wa maafisa utumishi wa mikoa, halmashauri na Taifa na sasa kazi hiyo ilishawasilishwa Ofisi ya Rais -Utumishi.
Dkt. Msonde ametoa wito kwa walimu kufanya kazi kwa kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu ya Tanzania sababu mwalimu ni mzazi na ndio mlezi na ili kuwa maendeleo mazuri ya nchi ni lazima kuwa na kizazi kilichoelimishwa katika elimu na maadili mazuri ya nchi yake.
Naye Mwl. Ackbaru Hema ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya walimu hasa yale Naibu Katibu Mkuu Elimu aliyoyasema ambayo ndio kilio kikubwa. Amesema wataendela kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha elimu ya watoto wa Tanzania inakuwa bora.
No comments:
Post a Comment