Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi Aisha Amour amewataka wakuu wa Taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kuanza kutumia mfumo wa kieletroniki katika ufanyaji kazi wao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kisekta.
Balozi Aisha, ameyasema hayo leo tarehe 15 Aprili 2024, wakati akifungua mkutano wa baraza la Wafanyakazi mkoani Morogoro.
“Niwatake kabla ya kuzindua mfumo, ndani ya wiki hii Taasisi zote ziwe zimeshaanza kutumia mfumo huu na muwaelekeze watu wenu wanaosimamia mifumo waanze kuingiza taarifa zenu zote” amesema Balozi Aisha Amour.
Vilevile, amesisitiza Wakuu wa Taasisi kuwa kwenye uzinduzi wa Mfumo kila Taasisi itatakiwa kuandaa na kuhakikisha taarifa zote muhimu zimewekwa kwenye mfumo huo.
Aidha, Balozi Aisha ameipongeza Bodi ya Mfuko wa barabara ( ROAD FUND),kwa kuwa Taasisi ya kwanza kuanza kutumia mfumo ambapo hadi sasa Taasisi imeshakamilisha kuingiza Taarifa zake zote.
Baraza la wafanyakazi la Wizara ya ujenzi, linafanyika Mkoani Morogoro kwa siku mbili lengo kuu ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali na kupokea wasilisho la Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 na mpango na makisikio ya Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2024/25.
No comments:
Post a Comment