Mfuko wa Mahakama umepokea shilingi bilioni 155.24 - NJENZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 30, 2024

Mfuko wa Mahakama umepokea shilingi bilioni 155.24 - NJENZA


Na Saida Issa,Dodoma

MWENYEKITI wa kamati ya Bunge ya Bajeti Oran Njenza amesema kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2024 Mfuko wa Mahakama ulikuwa umepokea jumla ya shilingi bilioni 155.24 sawa na asilimia 71.22 ya Bajeti iliyoidhinishwa.

Ambapo Kati ya fedha zilizopokelewa shilingi bilioni 50.13 zilitumika kwa ajili ya mishahara na shilingi bilioni 72.27 zilitumika kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.

Hayo aliyasema Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maoni ya Kamati ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Mfuko wa Mahakama kwa mwaka wa fedha 2023/24 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 202425.

Alisema kuwa Ufanisi katika utekelezaji wa bajeti ya matumizi mengineyo kwa asilimia 104 umetokana na mahitaji maalumu ya kugharamia majaji wapya walioteuliwa pamoja na kugharamia programu ya kuondoa mlundikano wa mashauri.

"Kwa upande wa fedha za maendeleo, fedha zilizopokelewa ni jumla ya shilingi
bilioni 32.84 sawa na asilimia 38.74 ya Bajeti,Kati ya Fedha hizo shilingi bilioni 3.65 ni fedha za ndani na shilingi bilioni
29.19 ni fedha za nje,"alisema

Aidha alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2023/24 Mfuko wa Mahakama ulipanga kukusanya maduhuli yenye jumla ya shilingi bilioni 12.57 ambapo Hadi kufikia Machi, 2024, jumla ya shilingi bilioni 7.54 zilikusanywa sawa na asilimia 60 ya lengo.

No comments:

Post a Comment