Mjukuu wa Bob Marley tangu aachie ngoma yake ya 'Praise Jah in the Moonlight. YG, ambaye ni mtoto wa Lauryn Hill na Rohan Marley, ameitingisha dunia kutokana na ngoma yake hiyo kufanya vizuri sana kila mahali.
Akiwa na umri wa miaka 22 tu, YG kupitia wimbo wake wa 'Praise Jah in the Moonlight, ameandika historia kwa kuwa wimbo wa kwanza wa reggae kufikisha streams bilioni 1 duniani kote.
Wimbo huo ambao ameuandika kwa kushirikiana na mama yake, Lauryn Hill, umepata mafanikio makubwa katika streaming za mitandao, zilizoufanya ufike hadi Na. 34 katika chati za Billboard Hot 100.
Akitumbuiza na mama yake Lauryn Hill. |
Mchango wa Lauryn Hill katika wimbo huo, kuanzia mashairi na hadi kurekodiwa, umetambuliwa na
mashabiki wake ukitajwa kuwa moja ya sababu za mafanikio ya jumla ya wimbo huo.
Lauryn Hill ambaye alitamba na kundi la Fugees miaka ya 1990 akiwa na wanamuziki wenzake wa Wyclef Jean na Pras, ameshiriki kidogo katika video ya mwanaye huyo ya wimbo 'Praise Jah in the Moonlight'.
"Praise Jah in the Moonlight" uliachiwa Desemba 27, 2023, lakini ukaanza kubamba mwishoni mwa Januari na mwanzoni mwa Februari 2024.
Mwezi Machi, wimbo huo ukatinga katika Top 10 ya TikTok Billboard Top 50 na kushika Na.2 baada ya kubamba sana katika mitandao ya kijamii.
Wimbo huo ni sampo ya wimbo
"Crisis" wa Bob Marley na kundi lake la
The Wailers.
Wimbo huo uliongezeka umaarufu baada ya binti wa Kim Kardashian na Kanye West aitwaye North West alipoutumia wimbo huo katika video yake ya TikTok, ambayo iliangaliwa mara milioni 30.
Staa wa Internet, Leah Halton aliposti video akiuimba kwa kufuatisha mashairi katika TikTok, ambayo ikawa moja ya video maarufu zaidi katika mtandao huo imetazamwa mara milioni 776.6 na ikapata 'likes' milioni 49.5 kufikia leo.
Lauryn Hill na Wyclef Jean wakimpa sapoti YG Marley. |
YG Marley amekuwa akifanya ziara mbalimbali za maonyesho akiwa na mama yake ikiwamo kutumbuiza Jamaica na Marekani.
YG Marley, ambaye jina lake halisi ni Joshua Omaru Marley, ni kati ya kizazi cha tatu cha Marley ambao
wanaendelea kuwasha katika muziki.
Wakati wa sherehe ya bethidei ya Jo Mersa Marley, nyota kadhaa wa kizazi kipya cha Marleys walioanda stejini kutumbuiza akiwamo motto wa Damian "Ir. Gong" Marley, Christian Marley, Mystic Marley, Zuri Marley, na Yohan Marley.
Marafiki wa familia katika muziki wa reggae kama Buju Banton, Sizzla Kalonji, Capleton, Spragga Benz, na wengine wengi walihudhuria na kutumbuiza.
Muziki wa Bob Marley pia umeuzika sana kupitia 'streaming' ya mtandaoni katika wiki kadhaa zilizopita soko ambalo limeamshwa na mafanikio ya
filamu ya maisha ya Bob Marley: One Love biopic.
YG Marley akiwa na mama yake, Lauryn Hill na baba yake, Rohan Marley. |
Kwa mujibu wa Box Office Mojo, filamu hiyo imeongoza kwa kuingiza Dola 89 milioni katika US box office kufikia Machi 10, 2024, na jumla imeingiza Dola 160 milioni duniani.
Mijadala ni mingi kwamba wimbo wa YG wa 'Praise Jah in the Moonlight, ulipaswa kuwania tuzo ya Grammy ya Wimbo Bora wa Mwaka.
Sehemu ya mashairi ya wimbo huo ambao ndio wimbo wa reggae unaotingisha dunia kwa sasa yanasema:
"Wanasema jua linawamulikia wote, Lakini kwa baadhi ya watu duniani haliwapi chochote,
Hii miale yote inawaka moto, ahh Kuonyesha kwamba nilikupenda, lakini bado unaniita mwongo.
Oh, no, no, no, no, no.."
No comments:
Post a Comment