"Nendeni mkawe wachungaji wema katika familia kama Bibilia inavyo elekeza kila mtu ni mchungaji kwa nafasi aliyonayo hivyo fundisheni yalio mema na sio matendo mabaya ambayo ni kinyume na maadili."
Kauli hiyo imetolewa Aprili 21, 2024 na Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Dodoma SACP Theopista Mallya wakati akizungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikra Maria Kisasa alipo shiriki ibada ya pamoja.
"Baba, Mama, Mlezi ongea na mwanao tuna kampeni yetu Jeshi la Polisi inayosema Familia Yangu Haina Mhalifu inatukumbusha kuhakikisha kuwa familia uliyopo hakuna mhalifu na kuepuka kushirikiana na wahalifu" amesema Mallya.
Kamanda Mallya amesema ili jamii iweze kuwa na aman ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kila Kata, Tarafa, Wilaya na familia aliyopo inakuwa salama kwa kuzuia sambamba na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha, Kamanda Mallya amewataka viongozi wa dini wa madhehebu yote pamoja na waumini kukemea vitendo viovu ambavyo ni kinyume na maadili vinavyo pelekea kuwepo kwa uhalifu katika jamii hususani vitendo vya ukatili na unyasasaji.
Katika hatua nyingine Kamanda Mallya amechangia ujenzi wa Kanisa unaondelea kanisani hapo kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja fedha itakayotumika katika uwekaji wa kioo kanisani hapo.
Pamoja na hayo, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kisasa Padre Sostenes ameshukuru Jeshi la Polisi kwa kuwaunga mkono kwa kuchangia hatua za ujenzi wa kanisa hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Jeshi La Polisi na kusimama imara katika kukemea vitendo viovu. ambavyo ni kinyume na maadili.
No comments:
Post a Comment