TARURA INAFANYA KAZI KUBWA YA KUGUSA MAISHA YA WATU- MHE. KATIMBA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 9, 2024

TARURA INAFANYA KAZI KUBWA YA KUGUSA MAISHA YA WATU- MHE. KATIMBA.



Dodoma


Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewapongeza  mwakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) kwa kazi kubwa wanayofanya ya kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunganisha barabara za wilaya nchini.


Mhe. Katimba ameyasema hayo  leo Aprili 9, 2024 alipokutana na kufanya kikao na menejimenti  ya TARURA kwenye ukumbi wa wakala uliopo mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.


Amesema TARURA inafanya kazi kubwa ya kugusa maisha ya watu na ustawi wa jamii kila siku kwani barabara wanazozijenga zinaenda kutoa Huduma za kijamii pamoja na zile za kiuchumi.


“Watanzania wana matarajio nasi, hivyo mjipange na kuwe na jitihada za kuleta suluhishi hususan msimu wa mvua”. 


Hata hivyo amesema waendelee kuwa wabunifu, washirikiane na kutatua changamoto pale panapotokea dharura.


Naye, Mtendaji mkuu wa TARURA mhandisi Victor Seff amesema wamefanya kazi kubwa ya kurudisha mawasiliano  maeneo yaliyokumbwa na Elnino hususan  maeneo ya kutolea huduma za kijamii.




T






No comments:

Post a Comment