Walichofanya Klabu ya Yanga ni kutocheza na shilingi chooni, wakaamua kutoa mkataba wa muda mrefu kwa Kiungo Mshambuliaji wao, Stephane Aziz Ki ambao utamuweka jangwani kwa miaka mingine mitatu.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Aziz Ki ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari ameshasaini mkataba na Yanga na kilichobakia ni kuweka hadharani juu ya makubaliano hayo.
Mkataba wa awali wa Aziz na Yanga unafikia ukingoni Juni 2024, na amehusishwa na vilabu vya Afrika Kusini ikiwemo Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates zote zikihitaji huduma ya kiungo huyo wa Burkina Faso.
No comments:
Post a Comment