WAKALA AFUNGUKA JUU YA CHE MALONE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 10, 2024

WAKALA AFUNGUKA JUU YA CHE MALONE.



Wakala wa Beki wa Klabu ya Simba, Che Malone, Amadou Fontem Tigana, amesema beki huyo hajasema kuwa haipendi Simba na wala hajasema kuwa anataka kuondoka Simba, bali watu wamemtafsiri vibaya mchezaji huyo.



Tigana ameyasema hayo wakati akizungumza na ITV kwa njia ya simu, ambapo amesisitiza kuwa taarifa hizo ni uzushi kwani ametafsiriwa vibaya baada ya kusema kuwa atacheza Kwa juhudi ili klabu kubwa kama Simba zimnunue.



Uafanunuzi huo wa Tigana unafuata, baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mchezaji huyo amefanya mahojiano kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao na kwamba tayari ameandika barua ya kuondoka Simba na kwamba anatala akatafute changamoto kwenye timu kubwa.

No comments:

Post a Comment