Maafisa waliwataka watu kusafiri hadi kwenye uwanja wa ndege ikiwa tu wamethibitisha kuhifadhi. |
Maafisa waliwataka watu kusafiri hadi kwenye uwanja wa ndege ikiwa tu wamethibitisha kuhifadhi
Shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai bado zimetatizika pakubwa baada ya mvua kubwa kunyesha katika Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi jirani.
Dhoruba hiyo kali iliipiga UAE siku ya Jumanne, na kusababisha barabara maji kwabarabara na sehemu za uwanja wa ndege wa kimataifa wenye shughuli nyingi.
Mafuriko makubwa sasa yameua watu 20 nchini Oman na mmoja katika UAE.
Baadhi ya safari za ndege za ndani zimeanza tena Alhamisi, lakini katika uwanja mzima wa ndege wa kimataifa wa Dubai, kituo kikuu cha usafiri, kinatatizika kufanya kazi.
Maafisa wamamlaka katika uwanja huo wa ndege wa pili kwa shughuli nyingi zaidi duniani siku ya Alhamisi walisema kwamba walikuwa wameanza kupokea safari za ndege zinazoingia ndani katika Terminal 1, zinazotumiwa na wachukuzi wa kigeni, lakini safari za nje zinmeendelea kuchelewa.
No comments:
Post a Comment