AWESO AITAMBULISHA PROGRAMU YA UCHIMBAJI WA VISIMA 900 VIJIJINI - OKULY BLOG

Breaking

Home Top Ad

TANGAZA NASI HAPA | PIGA 0785 364 965

Saturday, May 4, 2024

AWESO AITAMBULISHA PROGRAMU YA UCHIMBAJI WA VISIMA 900 VIJIJINI


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameitambulisha rasmi programu ya uchimbaji visima 900 kwenye majimbo 180 ya vijijini katika kijiji cha Maescron Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara aliposhughudia kisima cha kwanza kikichimbwa.

Wizara ya Maji kupitia RUWASA inatekeleza programu maalumu ya uchimbaji visima 900 ambavyo vitachimbwa katika majimbo 180 ya vijijini kwa visima vitano kwa kila jimbo kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji.


Programu hiyo ambayo imelenga kupunguza kero ya uhaba wa maji kwenye maeneo ambayo hayajifikiwa na huduma.

Utaratibu wa uchimbaji wa visima hivyo ni maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kumtua mama ndoo kichwani.

Utekelezaji wa mpango huu unategemea fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia programu ya P for R, Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) pamoja na Wadau mbalimbali.

Aidha, Programu hii kwa ujumla wake inatarajiwa kutumia zaidi ya ya shilingi Billioni 54.

No comments:

Post a Comment

HABARI KUU KWA SASA

  Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Nickson Simon John amelipongeza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kupitia kikosi chake cha Ruvu JKT kwa kuendelez...